Tatizo la Mabaka, Mba na Fungus (Fangasi) sugu na kuwashwa sehemu za siri kwa wanaume na wanawake- Fahamu chanzo, Dalili na Matibabu yake

Mkuu, kuhusu dawa ya Septrine ya shilingi 1000, wauzaji wengi huuza dawa kwa dozi. Je, nikinunua dozi 1 nitumie vidonge vingapi? au nitumie dozi nzima kwa kopo dogo la sh. 300 la vaseline? Ufafanuzi tafadhali.
 
Nimeipenda hii Ndugu
How about dosage and duration?
 
Nimeipenda hii Ndugu
How about dosage and duration?
Duration ni mpaka upone, but within three days utaona mabadiriko, dosage ni septrin za buku changanya na bby care mafuta. Paka twice per day hasubuhi na jioni
 
Nakushukuru sana youngkato nilitumia hiyo septrine ya 1000 na mafuta ya vaseline nilikuwa na fangas sugu mguu wa kulia kwa zaidi ya miaka 10 nimepona, asante sana Mungu akubariki.
Ulifanyaje ndugu sobya? Hiyo Septrine ya shilingi 1000 inakuwa na vidonge vingapi? Na vaseline ya shilingi 300 ina ujazo kiasi gani? Tafadhali naomba ufafanuzi ili nisije kuzidisha au kupunguza katika uchanganyaji. Asante.
 
Ulifanyaje ndugu sobya? Hiyo Septrine ya shilingi 1000 inakuwa na vidonge vingapi? Na vaseline ya shilingi 300 ina ujazo kiasi gani? Tafadhali naomba ufafanuzi ili nisije kuzidisha au kupunguza katika uchanganyaji. Asante.
Septrin Ni kama vidonge kumi, na mafuta kikopo kidogo kabisa ni kama gram 25. Ila hakuna ratio maalum ya huo mchanganyiko la muhimu ni kuona ile dawa uliyopaka imesambaa sehemu unayoumwa
 
Anthony, unakwenda duka la dawa unaomba kuuziwa septrine za 1000 na mafuta ya vaseline madogo kabisa au baby care kama alivyoshauri youngkato (daktari wetu ) unazisaga septrine mpaka zinakuwa unga bila chenga hata kidogo, unachanganya na hayo mafuta, vikichanganyika unapaka kwenye ugonjwa asubuhi na jioni. Pole, tumia dawa utapona.
 
Asante. Nitazingatia maelekezo.
 
Yawezekana una 'genital herpes'... and not fangasi. Pole mrembo.

-Kaveli-
 
nenda hospitaly kubwa ukaeleze matatzo yako yote bila kuficha mpaka hapo ulipo then ufanyiwe vipimo tatzo lako lijurikane
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…