Tatizo la Askari wetu linaanzia mbali sana. Wanahitaji msaada mkubwa sana. Matukio haya yanatisha

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
Nikikumbuka tukio la Nape na hili la Malima naona kuna shida kubwa sana ambayo kama Serikali isipoingilia hapo mbeleni kutakuja kutokea Mauaji.

1. Askari wetu wengi ni Form Four Failures kwa asilimia 80. Hawa tayari katika uelewa wao wanajiona wameshadharaulika na jamii. Askari mmoja alikuwa akiongea tukiwa tumekaa sehem anasema "sisi ni kama mbwa tu,tukitumwa kung'ata tunaenda na raia wanatudharau sana. Hatupati madem wazuri/wakali. Raia wanatuona sisi ni watu wa daraja la chini sana" alizungumza kwa uchungu sana. Kisa ilikuwa kuna mtu alinisalimia kwa heshima na huyu jamaa hakusalimiwa nikamwambia huyu jamaa yangu ni askari. Akajibu tu ok. Hajaenda lindo. Kumbe hilo neno lilimkera sana. Akatengeneza hasira

2. Tumeona matumizi mabaya ya bastola au bunduki kwa askari.wanataka turudi miaka ile ya ukoloni ilikuwa tukimwona askari tunakimbia kujificha .lakini hili si lengo la askari nchini. Na ndo imesababisha raia wakikuta askari anapigwa wanamwacha apigwe maana askari wametengeneza uadui na raia.ubabe kila sehemu.

3. Askari wengi hawajui kujenga hoja ukitaka tu kumwelekeza jambo anakasirika anaona umemdharau bahati mbaya ukiweka na neno la kiingereza ndo umeharibu kabisa anakuona umemdharau sababu wewe umesoma. Haya ni moja ya matatizo makubwa sna kwa askari wetu.

4. Tunakoelekea askari atakuja kumshoot mtu halaf akasema alimdharau au wakasingizia ni jambaza. Tuliyaona kwa nape, tumeyaona kwa bwana malima, tutazid kuyaona. Kama wahusika wasipoliangalia hili wananchi watakuja kuasi. Umma una nguvu sana.tujifunze misri ilikuaje.
 
Ni kweli " Mwanzo wa ngoma ni lele lele"

Hii ni kauli ya JPM askari lazima waogopwe.Ngoja waogopwe Ika wakiuawa wasirudi kuuliza RAIA tena ni vyema wanarudi kwenye silaha na kuuliza kwanini wanauawa.

IGP asipokuwa makini la Uganda laweza kutokea.
 
Customer care na negotiations skills ni muhimu kwa askali wetu hasa katika kipindi hiki ambacho uelewa wa watu umeongezeka.
Unakuta mtuhumiwa anaonyesha ushirikiano wote lakni bado mtu anataka amkate mitama, amzabe vibao, au amlambe bakora.
Matrafic wengi naona wako vzr suala la mawasiliano.
 
Huyo askari siyo mzima na lazima kavuta bangi. Watanzania wengi ni askari wa akiba tumepitia JKT tumefundishwa silaha huwezi kutumia silaha kijinga vile. Yule kijana hafai kabisa kuwa askari na hafai kabisa kukabidhiwa silaha na nitashangaa sana kama ataendelea kukabidhiwa sikaha. Yule mwenzake aliyekuwa akimzuia anaonekana kuwa na busara sana.
 
Nikikumbuka tukio la Nape na hili la Malima naona kuna shida kubwa sana ambayo kama Serikali isipoingilia hapo mbeleni kutakuja kutokea Mauaji.

1. Askari wetu wengi ni Form Four Failures kwa asilimia 80. Hawa tayari katika uelewa wao wanajiona wameshadharaulika na jamii. Askari mmoja alikuwa akiongea tukiwa tumekaa sehem anasema "sisi ni kama mbwa tu,tukitumwa kung'ata tunaenda na raia wanatudharau sana. Hatupati madem wazuri/wakali. Raia wanatuona sisi ni watu wa daraja la chini sana" alizungumza kwa uchungu sana. Kisa ilikuwa kuna mtu alinisalimia kwa heshima na huyu jamaa hakusalimiwa nikamwambia huyu jamaa yangu ni askari. Akajibu tu ok. Hajaenda lindo. Kumbe hilo neno lilimkera sana. Akatengeneza hasira

2. Tumeona matumizi mabaya ya bastola au bunduki kwa askari.wanataka turudi miaka ile ya ukoloni ilikuwa tukimwona askari tunakimbia kujificha .lakini hili si lengo la askari nchini. Na ndo imesababisha raia wakikuta askari anapigwa wanamwacha apigwe maana askari wametengeneza uadui na raia.ubabe kila sehemu.

3. Askari wengi hawajui kujenga hoja ukitaka tu kumwelekeza jambo anakasirika anaona umemdharau bahati mbaya ukiweka na neno la kiingereza ndo umeharibu kabisa anakuona umemdharau sababu wewe umesoma. Haya ni moja ya matatizo makubwa sna kwa askari wetu.

4. Tunakoelekea askari atakuja kumshoot mtu halaf akasema alimdharau au wakasingizia ni jambaza. Tuliyaona kwa nape, tumeyaona kwa bwana malima, tutazid kuyaona. Kama wahusika wasipoliangalia hili wananchi watakuja kuasi. Umma una nguvu sana.tujifunze misri ilikuaje.
Tatizo hawajiulizi, imeshakuwa mbaya air!!
"
Kama wanaufanyia hayo mtu mbichi itakuaje kwa mti mkavu"Mwenyezi mungu huta mwona ili akuelekeze kwa kidole wake huta sikia sauti yake
Ishara ndiyo lugha yake serikali uchukue tahadhari
 
MTU anayemdharau polisi si Wa kumuonea huruma!! Ebu acha unafiki tena anabahati yule Askari ni mpole angekuwa mwingine kama [HASHTAG]#julio[/HASHTAG] angekuwa aahakula na makofi mengi sana pale....
Nyie ndio mnawaponza askari wetu mpaka yakiwafika watu wanaona ni kawaida. Askari lazima awe na weledi, hawezi kukasirishwa na maneno tuu kwani yaweza toka kwa mlevi. Hii inferiority complex waliyo nayo inavunja heshima ya jeshi
 
wanaboa achana nao.... kila kitu siasa... niheri ninavyowachukia polisi kuliko ninavyowachukia baba zao wanaojifanya wana own nchi na wako above the law.. Hunijui mimi ni nani?? Mwite bosi wako?? Mimi nilikuwa waziri?? what the h...
 
Nyie ndio mnawaponza askari wetu mpaka yakiwafika watu wanaona ni kawaida. Askari lazima awe na weledi, hawezi kukasirishwa na maneno tuu kwani yaweza toka kwa mlevi. Hii inferiority complex waliyo nayo inavunja heshima ya jeshi
wewe wape bichwa vigogo poli.... iko siku polisi kaamka vibaya hapigi juu anapiga kichwani
 
Back
Top Bottom