Tatizo la arusha


M

Mzee wa Usafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2008
Messages
642
Likes
102
Points
60
M

Mzee wa Usafi

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2008
642 102 60
Nikiwa kama Mtanzania mwingine anaye penda haki na amani iwepo kwa kila raia na mgeni hapa Tanzania napenda kusema kuwa tatizo Zima la Arusha lipo ndani ya Jeshi la Polisi. Ndani ya Jeshi la Polisi ukitaka haki itendeke basi wewe ni adui na unaunga mkono upinzani. Kwa nini nasema hivyo

1. RPC wote waliotekeleza kazi yao kwa haki wakati wa uchaguzi wa 2010 na kutofautiana na viongozi wa mkoa au wilaya wa CCM wote walihamishwa na kurudishwa Makao Makuu....Hapa ni RPC Basilio, RPC Sirro na wengine.

2. OCD wa Arusha mjini Bwana Zuberi amekuwa akitumiwa sana na Magamba na IGP Mwema kama kawaida yake ,baada ya mauaji ya raia wema wakati wa maandamano ya Chadema na tabu alizo kuwa akimpatia Mbuge Lema , alipandishwa cheo na sasa ni Staff Officer na kituo chake kipo hapo hapo Arusha.

3. OCD mpya mpenda haki na asiye taka kusukumwa na magamba Mponjoli alitofautiana na Zuberi baada ya Zuberi kuingilia majukumu ya OCD cha ajabu , Mponjoli alimbulia uhamisho wa kwenda Kanda Maalumu Rorya. Kwa namna hii ya utendaji unafanya raia wawe target ya kupandia ngazi na cheo kwa maafisa kwani inalipa kujipendekeza....Kumbuka kilichotokea kwa Kamuhanda


Ili Jeshi liaminike kwa wananchi wote ni lazima watu waliamini kuwa lina tenda haki..kwa sasa hakuna anaye liamini jeshi letu ispokuwa CCM na wafuasi wake.

Ushauri kwa MWema badili utendaji kazi wa timu yako....kwa sasa mnatupeleka kubaya
 

Forum statistics

Threads 1,273,280
Members 490,351
Posts 30,476,446