Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,655
- 2,003
Heshima kwenu wakuu. Nafika hapa jamvini kuomba magwiji wa Gadgetry mnisaidie kupata suluhisho la tatizo kwenye laptop yangu. Ni HP 250 G3 NOTEBOOK. Niliipata ikiwa brand new na ninayo mwezi wa pili huu. Ina Windows 8.1. Juzi nilikuwa nasurf internet mara nikaletewa alert kuwa kuna threat ya virus. Faster nikascan lakini baada ya hapo zile tiles kwenye Start screen zikapotea, Pc Settings hazifunguki tena, Bluetooth Settings hazifunguki tena na hata Web Cam haifunguki. Nimejaribu kufanya Non-destructive Recovery lakini haikusaidia. Naomba maelekezo nifanyeje kuirudishe katika hali ya kawaida bila kulazimika kung'oa windows kabisa.