OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Huu ni mwezi wa Wanawake duniani, basi na mimi nimeona niweke hoja za kuwasaidia kwenye kutimiza malengo yao ya usawa (Theoretically)
Takwimu zinaonyesha umasikini kuwa mwingi kwa jinsia ya kike, hii ni kutokana na wao kuwa wachache kwenye shughuli za kiuchumi
Sera ya elimu ya mwaka 2014 imeainisha takwimu zinazoonyesha uchache wa wanafunzi wa kike katika ngazi zote za elimu. Pia kitabu kinachotolewa na NBS, Women and Men Facts and Figures kimeonyesha wanawake ni wachache kwenye masuala ya kielimu, na pia kwenye ajira tofauti tofauti.
Swala hili ni la kusahangaza ukizingatia wanawake ni wengi kuliko wanaume nchini Tanzania.
Wakati wa maadhimisho haya ya mwezi wa wanawake ni vyema kuangalia msingi kwanza kabla ya kuangalia vitu ambavyo bila msingi bora vitapeperuka ndani ya muda mfupi. Katika ulimwengu utakao kuwa na idadi kubwa ya wasomi, ni wazi hata siasa na maeneo mengine ambayo yamehitaji usawa yatahitaji kuwa na wasomi, na kama wanawake watakuwa ni wachache katika ngazi za elimu ni wazi usawa wa kisiasa na kiuchumi utakuwa ni ombwe.
Katika kitabu hiko cha NBS wametoa mapendekezo ya kubadili sheria ya Mirathi ambayo imekuwa ni mwiba kwa mwanamke, pia sheria ya ndoa ambayo ilikuwa inaruhusu mtoto wa miaka chini ya miaka 18 kuolewa kwa idhini ya wazazi wake.
Mbali na mapendekezo hayo, ni lazima tujue hali ya wanawake kwa sasa ni swala la 'Mind set', mind set haibadiriki kwa sheria, sheria huongeza aidha rushwa au idadi ya watu wanaokwenda jela, na itakuwa ni shida ileile tu ya kusolve tatizo moja kwa kutengeneza tatizo lingine.
HOJA!
Swala la wanawake ni swala la kuanza kujadiliwa kwa ngazi zote kabla ya sheria(naweza kutetea hili) kwanza kwenye shule za wasichana, wasichana inabidi wajifunze thamani zao ili wao wawe mabalozi kwa wanwake wengine mtaani na kwenye matukio mbali mbali huko mtaani
Swala la mimba kwa wanafunzi liangaliwe kwa jicho la kitaalamu na mazingira, approach yangu kwa mimba kwa wanafunzi ni wazazi, walimu na wizara kuona umuhimu wa elimu ya jinsia na kuwafunza watoto kuhusu vyote vinavyohusu maumbile yao.
Sheria ya kuwaweka watu jela itazidisha umasikini, kama nilivyosema mwanzo kuwa sheria huongeza rushwa au idadi ya watu kwenda jela, ndivyo ilivyo kwa wanaowapa wanafunzi mimba. Mtoto wa kike anaacha shule, mwanaume anaenda jela, then what? wengine wajifunze?
Watu hawajifunzi kwa coercive means, bali elimu inayokuwa imparted kwa utaalamu mkubwa, tafiti zinaonyesha uwepo wa capital punishments hakujawahi kuleta mabadiliko yoyote kwa watu.
Masuala ya wanawake yajadiliwe kitaalamu, na waweke misingi ya matatizo yao na sio kudeal na matokeo na kuacha sababu halisi ya matatizo yao. Kuvaa mat-shirt, kuandamana, kula pamoja au kutoa michango hakutoshi kama kwanza hayatajadiliwa yanayozaa haya yote.
KAULI KUU, YANAANZA NA ELIMU
TUANZE NA ELIMU
Signed
OEDIPUS