Tathimini ya Safari kutoka Njombe kwenda Mbeya(231km) kwa kutumia pikipiki

bush crazy

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
757
1,020
Habari wanabodi!
Hivi karibuni nilisafiri na pikipiki Njombe to Mbeya. Safari ilinigharimu takribani masaa sita. Lengo la Safari Lilikuwa ni kutalii. Aina ya pikipiki Ni T-Better 150 toleo la 2013.
Nilichogundua pikipiki hizi si rafiki kwa Safari ndefu.

MCHANGANUO WA VITUO NILIVYOPUMZIKA NA MUDA NILIOTUMIA.

Nimeindoka njombe saa 12.30
Nimefika. Makambako Saa 1.27
Nimendoka saa 2.50
Nimefika igawa saa 4.10 asubh
Nimendoka. Saa 4.27 asbh
Nimefika igurusi saa 5.37
Nimendoka saa 5.50
Nimefika uyole saa 6:46 mchana

USHAURI
Pikipiki Ni hatari kwa afya kuwa makini ukiwa safarini
Tumia pikipiki zenye nguvu katika Safari ndefu.
Msimu wa kiangazi ni mzuri kwa Safari ndefu za pikipiki.
Nilitumia Lita 6
Average speed 60km/ 1hr

HITIMISHO:
Mungu anipe uzima mwaka 2021 ikipendeza nitasafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha kupitia Dodoma. Nikiwa na Boxer BM 150.

IMG_20201228_095539_6~2.jpeg
View attachment 1663892
 
Mi naona usafiri wa pikipiki sio hatari kama utachukua tahadhar zote za usalama barabarani. Pia usishindane na magari. Pia kama huna mzigo ulopakia inakubididi uslow down unapopishana na mabasi au maroli.

Mimi niliwahi kusafir na boxer 150, mwaka 2015 kutoka mwanza kwenda geita kupitia kigongo feri n nikarudi siku hiyohiyo jioni. Ilikua poa sana na niliyafaidi mazingira mazuri ya kanda ya ziwa.
 
Hakika mkuu Cha msingi tahadhari zote Kama kunguru .
 
Bro una picha za gears ulizovaa?
Vaa Sweta leta chestcover then tupia bonge la koti. Vaa jinsi isiyobana then kwa nje tupia suruali la track suit inayozuia upepo kuingia kwenye mifupa. Mikononi tupia gloves za kisela. Hakikisha pikipiki yako ina Bima, Sumatra(Latra) + stika ya nenda kwa usalama ambazo mwaka huu hazijatoka. Ukifika baadhi ya miji wanaushuru wa maegesho hakikisha unalipa kabla hawajakudaka maana huwa hawana huruma Hawa mawakala.
 
Back
Top Bottom