Taswira ya Nchi (Tanzania) ni Inatisha Kwa Sasa

EWGM's

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
1,521
2,112
Inchi yetu ilikuwa na amani na utulivu na uhuru wa kufanya mambo ingawa si kwa "..to that extent" lakini sasa imeingia woga na hofu kubwa mitaani. Sitazungumzia swala la kiuchumi na ishara zote mbaya za kibiashara ila nitakijita kwenye "Hofu".

Inchi hii kwa sasa imefata mfumo wa nchi za Kisoviet ambao kwa sasa hawana tena nguvu ya kuweka vita baridi kwenye nchi nyingine ila imekuwa inatumia cyber system kudhoofisha nchi pinzani na "fake news". Wanatumia mfumo wa kibabe na "divide and rule" na hii ni mrejesho baada ya muungano wao wa Kisoviet kuvunjika.

Walianza na Brexit kwa nchi ya Uingereza, akafata Trump nchini Marekani japokuwa walishindwa Uholanzi sasa wameelekeza nguvu kubwa sana Ufaransa kwa sasa na ikifatiwa na Ujerumani kwenye ramani.

Ila kwa Tanzania kwa sasa tunatumia kuna vijana wamejitolea wanatumia mfumo uleule ila si wa kimataifa bali kitaifa. Kuna vikundi ambavyo vimeshaota mizizi mikubwa na kuweza kutoa propaganda kwenye mitandao kutia hofu jamii kuwa unapokuwa na mtazamo tofauti na serikali au chama fulani basi utapotea, utaona cha mtema kuni au utashughulikiwa.

Kikubwa kundi hili moja lina nguvu kubwa na linatia woga wananchi, kusambaza habari za vitisho na kuivika serikali au chama fulani nguvu ambazo kiukweli haina. Tumeona mengi kuanzia kutumbuana, fine za Mil. 7, Kudhalilishana kwa majina kwenye jamii, uvamizi na sasa utekaji. Ila kikubwa ni hawa askali pandikizi walio mstari wa mbele "new frontiers" wa kusambaza habari za kuzusha, kutoa vitisho kwenye mitandao pamoja na hiki kikosi maalum cha utekaji.

Hawa "Frontiers" wa "fake news" wameleta hofu kubwa na kubadili ukweli kuwa uwongo au uwongo kuwa ukweli. Mfano utekwaji wa Roma Mkatoliki wanatumia nguvu kubwa kuweza kuiaminisha jamii ni Roma mwenyewe alitengeneza ule mchongo. Sijajua kama kuna mtu nchi hii anaweza kujiweka kwenye maumivu na mateso makali namna ile ili aje ajitengenezee kiki.

Kwa kufanya hivyo kwanza ni kosa la jinai na kusababisha matumizi mabaya ya nguvu na rasilimali za jeshi la polisi kutumika pasipo hitajika. Ikija kudhitika bila shaka kwamba Roma Mkatoliki alijiteka mwenyewe nitakuwa wakwanza kuomba msamaha kwa yale yote niliyasea au andika kuhusiana na tukio zima.

Sasa je, ni nini kifanyike ili kuweza kuliondoa ongwe hili la hofu liliotanda ndani ya nchi yetu? Tunaomba tuchangie kistaarabu na kuleta suruhu ya kufanya hali ya utulivu na amani irudi nchini na nchi iweze kwenda mbele na kufanikisha yote tunayoadhimia kama taifa.
 
Sasa kilanja mkuu na mlinzi wa raia na nchi anafanya nini ofisini wakati watu wanaleta hofu hii???
 
Nchi hii umetulia sana. Ila kwenye maneno ya mitandaoni ndio haijatulia. Naamini hata hao wa mitandaoni watatulia. Ndugu usiache kufanya issue zako kwa maneno ya mtandaoni. Utakuwa lofa!
 
Moderator wameacha habari gani ya uongo mkuu?

Mkuu soma maelezo pale juu ni wahusika tu ndiyo watakaojulishwa kama wakihitaji. Sisi tujadili nini kifanyike Hofu iondoke nchini hata simu sasa hatupigiani kwa woga, hatuongei siasa kabisa hofu
 
Sasa je, ni nini kifanyike ili kuweza kuliondoa ongwe hili la hofu liliotanda ndani ya nchi yetu? T
Tatizo ni hilo Dubwasha lenye Vyeti fake... Hakuna kingine. Na nchi haitatulia mpaka liondoke....
 
Nchi hii umetulia sana. Ila kwenye maneno ya mitandaoni ndio haijatulia. Naamini hata hao wa mitandaoni watatulia. Ndugu usiache kufanya issue zako kwa maneno ya mtandaoni. Utakuwa lofa!
Maneno ya mtandaoni au vitendo vya mitaani. Waliopotea wapo si hadith ya kuhadithiwa, waliokamatwa na kufungwa bila makosa wapo, waliokamatwa na polisi na kunyimwa dhamana wapo, wanaotishiwa maisha wapo. Si mambo ya mitandaoni ni mambo ya mitaani na yanayojili
 
Tatizo ni hilo Dubwasha lenye Vyeti fake... Hakuna kingine. Na nchi haitatulia mpaka liondoke....

Japokuwa na kuwa na dubwana la vyeti feki ninachoona mimi watu tuna-react badala ya tu-respond na hali halisi ili suruhisho lipatikane.
 
Japokuwa na kuwa na dubwana la vyeti feki ninachoona mimi watu tuna-react badala ya tu-respond na hali halisi ili suruhisho lipatikane.
Sasa unataka nini kifabyike.... Leo hii kabisa sjui nini kimetokea... Inspector ametoa wimbo wa. Kumtukana Roma..

Kama ulivyosema watekaji wapo kazini wanafanya kila wanaloweza ionekane ndivyo sivyo... Mbaya zaidi watu nao wanaanza kosa msimamo,, eti Roma alijiteka.

Serious, !??? Yani mtu asababishe maumivu kwa familia yake namna ile.... !??

Sisi wa Tanzania ni viumbe wa ajabu sana.
 
Tunakoelekea sio kuzuri.Naona hakuna kiongozi yeyote mwenye uthubutu.Wote wamelowa .Ninani wa kumjaribu mkulu?

Nape amempa ushauri mzuri tu ila la kuunda tume siliafiki wakorofi wanajulikana awajibishe ila ikishindikana wananchi tuamue nini cha kufanya nchi ni yetu sote.
 
Mkuu soma maelezo pale juu ni wahusika tu ndiyo watakaojulishwa kama wakihitaji. Sisi tujadili nini kifanyike Hofu iondoke nchini hata simu sasa hatupigiani kwa woga, hatuongei siasa kabisa hofu
mimi mdau wa JF na naona habari za uongo zinaondolewa, ziwe za upinzani au za serikali....
 
Back
Top Bottom