Kodi lazima walipe, na matumizi ya EFD lazima yawe ya kudumu. Hatuwezi kuwa Taifa la walipa kodi wachache na wengi wao wawe ni ujanja-ujanja tu. Lazima kodi zilipwe. Kenya wamefanikiwa sana kwa kutumia EFD. Hapa suala la bei za hizo mashine ni kisingizio tu. Watanzania hatuna utamaduni wa kulipa kodi. Nasema, kodi lazima ilipwe. Kwa sasa walipa kodi nchi hii ni walio kwenye ajira rasmi tu! Mtu anauza tv 10 kwa siku halafu anagoma kulipa kodi! Haiwezekani. Hata kwa kutumia virungu, lazima kodi ilipwe tu! Tukimaliza hiyo hatua, ndipo tuingie hii nyingine ya matumizi ya fedha za kodi, maana kuna genge la wachache ambao kazi yao ni kula tu. Kwa sasa TRA wanakusanya Sh bilioni 700 kwa mwezi, lakini wafanyakazi hawapati mishahara. Hilo liwe jukumu la pili baada ya kuhakikisha kila mmoja analipa kodi kwanza!