DOKEZO Responded TASAF walengwa hawafikiwi na misaada kwanini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu,


Kwanza, pole kwa huyo mlengwa. Kuna receipt zinazoonyesha kiasi alichokipokea. Je, imeandikwa kiasi gani? Au umemsikiliza tu kuwa huwa anapokea kiasi hicho? Ungejiridhisha kwa kuangalia malipo yake katika awamu husika.

Pili, kiwango kinatofautiana kati ya Kaya na kaya, kutegemeana na idadi ya Wategemezi. Kama hana mtegemezi (kwa kipindi hiko), alikuwa analipwa 24,000 kwa miezi miwili. Wategemezi wana kiwango chao. Mfano watoto wanaosoma sekondari wana kiasi chao, wanaosoma msingi pia wana kiasi chao.

Lakini pia, huwa wanafuatilia. Kuna watu wanaandikisha watoto wanasoma lakini watoto hawahudhurii shuleni. Wakipitia wakiona, wanamuondoa.

Tatu, hela za TASAF hazina makato. Kuna njia tatu, wanaopokea CASH ambayo serikali inataka kuifuta kabisa kwa sababu ina mlolongo usioridhisha. Kuna wanaopokea kwa njia ya OTC, ambapo hawa wanaweka kidole na namba za NIDA na taarifa zao kusoma kwenye mfumo na hela kutoka papo hapo. Alafu wanaopokea kwa njia ya simu na bank. Huwa wanawekewa hela ya Makato.

Kama anapokelea benki, huko kuna makato na hata charges za mwezi husika. Sijajua kama benki washirika zilifikia muafaka wa kutengeneza akaunti maalum kwa kaya maskini.

Nne, alipokuwa anasaini kupokea fedha aliona ameandikiwa kiasi gani? Miezi yote haifanani, kwa sababu kuna wanaolipwa kiasi ambacho labda hawakuchukua dirisha lililopita. Lakini kwa muktadha wa 30,000 si sahihi.

Nini cha kufanya?
Kwanza, soma receipt yake. Jihakikishie hela iliyoandikwa. Angalia pia aina ya njia anayopokelea. Kisha trace, kama ni CASH imekula kwake. Kwa sababu huna uhakika wewe au yeyote kuwa kweli alipokea kiasi hicho.

Nilishafanya kazi nao, umaskini upo kwenye fikra zaidi. Mtu anachukua hela, anahakiki kisha anasaini. Lakini anafika sehemu anapiga gongo alafu anarudi hela haijatimia.

Kama ni njia ya benki, muombe receipt ya kutoa hela. Kama imetoka 12,000 basi. Kama hana basi Wakala kamgonga. Vivyo hivyo kwa simu, kagua miamala yake.

Kama zote zipo sawa, nenda naye ofisi ya Mtendaji wa Kata. Akajaze form maalum ya rufaa ya kutoridhika na kiasi husika. Mtendaji atawasilisha rufaa yakee manispaa na wao watawasilisha HQ.

Pia, mueleweshe hiyo hela ni ruzuku. Asilie sana. Ni huruma ya serikali. Akumbuke baada ya miaka mitatu anapaswa kutoka aingie mwingine.
 
Mkuu mtu katoka ofisini na unamuona ana kuja na 12000 kakatwa unasema nini au unataka nikutajie kijiji?

Pia kushtak kwa mendacious wakat wao pia ni wale wale
 
Karatasi aliyopewa i wapi?
Anapokea cash na kuhus karatas anayo mwenyewe ila ukweli ni kwamba ninyi mnawapiga wananchi mnakula hela za wananchi kwakivuli cha kuwasaidia na kuwaweka watu wasio husika ukiata evidence kabis nitakupa location sio kijiji kimoja kina walalamikia
 
Nchi watu ni wezi by nature

Ova
Na ndio watu hao hao ambao wanaka kwenye tv wengine wakiruka sarakasi bunge kuonyesha wanaumia kuhusu umasikin wa wananchi wengine ndio hao msukuma kala honey hana kelel
 
Vigezo vya kuingia Tasaf ni vipi? Mbona kila nikiomba hawanipi, nakati naona nina kila haki..
 
ila ukweli ni kwamba ninyi mnawapiga wananchi mnakula hela za wananchi kwakivuli cha kuwasaidia na kuwaweka watu wasio husika
Umenikosea sana Mkuu.

Ninyi? So, I am within them robbers.

Mungu akusamehe. Nilikuwa natoa maoni ni kwa namna gani unaweza kumsaidia kujua tatizo nini ili apate msaada. .

Ila allegations zimenigeukia mimi.
 
Umenikosea sana Mkuu.

Ninyi? So, I am within them robbers.

Mungu akusamehe. Nilikuwa natoa maoni ni kwa namna gani unaweza kumsaidia kujua tatizo nini ili apate msaada. .

Ila allegations zimenigeukia mimi.
OK sorry ila hao majamaa ni wezi ilo usikatae mkuu
 
Atakumbukwa kwa kauli ya kuleni kwa urefu wa kamba zenu,akatahadharisha kua wasile hadi kuvimbiwa.Ile kauli bilashaka aliteleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…