Tarime wamuomba Heche kugombea ubunge

Tarime wamuomba Heche kugombea ubunge

Kalesya

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2014
Posts
691
Reaction score
728
Katika hali inayoonyesha kuzidi kung'aa kwa nyota ya John Heche Kisiasa, kwa mara nyingine tena wakazi wa jimbo la uchaguzi la Tarime mkoani Mara wamemuomba kijana wao huyo agombee Ubunge jimboni humo kwasababu ni kijana wanayemuamini sana katika kupambana na udhalimu katika kipindi hiki cha ukombozi mpya wa Taifa hili.

Hayo yote yameonekana katika kipindi chote ambacho Heche amekuwa katika harakati za kisiasa hapa nchini, tangu akiwa mwenyekiti wa BAVICHA na mpaka sasa.

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti na mitandao ya kijamii imewanukuu wananchi wa Tarime wakimuomba kijana wao huyo kulinyakua jimbo hilo bila kusita.
attachment.php

 

Attachments

  • IMG-20150123-WA0002.jpg
    IMG-20150123-WA0002.jpg
    222 KB · Views: 544
  • IMG-20150126-WA0006.jpg
    IMG-20150126-WA0006.jpg
    65.5 KB · Views: 542
  • IMG-20150113-WA0005.jpg
    IMG-20150113-WA0005.jpg
    160.6 KB · Views: 2,539
Hakuna ubishi, Heche anafaa kuliongoza jimbo la Tarime.
 
Heche hawezi chochote na hana lolote mdogo wangu yule hajiwezi kabisa

KAKA YAKO NAPITA; jitahidi kuwa na free mind; ukisema hajiwezi kabisa una maanisha nini? mbona tumeona jinsi alivyoiongoza BAVICHA kwa mafanikio kabisa! lakini wote tumeona jinsi alivyopambana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na matokeo yake tumeyaona, sasa sijui wewe umeona hajiwezi ki vipi, Heche kama unania hiyo ya kugombea ubunge TARIME endelea nayo unaweza na ninauhakika ukipenya kwenye chama chako, kwa wananchi tayari wewe ni mbunge unayesubiri kuapishwa mwezi november.
 
Wananchi wa Tarime wanahitaji mtu sahihi atakae wakomboa na kuwaletea maendeleo,ndio maana wakaona kijana wao mpendwa, zao lao, John Heche ndio mtu sahihi wa kutimiza malengo yao. Big up wana Tarime kwa kuliona hilo.
Kamanda Heche sikiliza kilio cha jirani zako,ndugu zako, wazazi wako, wadogo zako, vijana wenzio Wana Tarime.
 
Huyo aliesema hajiwezi,akagombee yeye,,anaejiweza.
 
Nadhani Logistics tayari kati ya Mwita na Heche.
Mwita tayari ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa jijini dar.
Nadhani atagombea hukohuko dar,nafikiri Segerea!
Heche atagombea Tarime.
Hamna haja ya kuchochea ugomvi.
Subirini wapambe wa MWIKABE WAITARA waje.
 
Heche hawezi chochote na hana lolote mdogo wangu yule hajiwezi kabisa

Acha wivu na uzembe! Heche anaweza na hilo ni kwa mujibu wa wananchi wa Tarime wenyewe siyo wewe binafsi. Mbaya zaidi huna hoja ya kuulinda mtazamo wako hasi, hivyo basi wewe ndo huwezi kitu.
 
Subirini wapambe wa MWIKABE WAITARA waje.

Chadema hakuna historia ya kugombania majimbo, matakwa ya wananchi husika ndicho kigezo kikuu cha uteuzi ndani ya chama kuanzia kamati ya utendaji ya Wilaya mpaka kamati kuu Taifa kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za CHADEMA. Ni suala la muda tu kujua Mwita Waitara atahitajika na Wananchi wa jimbo gani.. Wote hawa ni Makamanda wapiganaji. Mwita analisukuma gurudumu la maendeleo Kivule pale Ukonga.
 
binafsi sina namna ya kuzuia wananchi wasiseme
lolote lakini nashauri chama chao kiwe makini sana na CCM kwa sasa CCM wanachopanga ni namna ya kugawa wagombea ile TARIME inamuhitaji mtu kama HECHE ni kijana anayejituma kwa kweli
 
Hilo jimbo si lina mbunge? Nyambari ni mbunge wetu mpaka aache mwenyewe
 
hyu heche ni j3mbe haswaaaaaaa magamba kina rits na beno maliza wanamtambua
 
katika hali inayoonyesha kuzidi kung'aa kwa nyota ya john heche kisiasa, kwa mara nyingine tena wakazi wa jimbo la uchaguzi la tarime mkoani mara wamemuomba kijana wao huyo agombee ubunge jimboni humo kwasababu ni kijana wanayemuamini sana katika kupambana na udhalimu katika kipindi hiki cha ukombozi mpya wa taifa hili.

Hayo yote yameonekana katika kipindi chote ambacho heche amekuwa katika harakati za kisiasa hapa nchini, tangu akiwa mwenyekiti wa bavicha na mpaka sasa.

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti na mitandao ya kijamii imewanukuu wananchi wa tarime wakimuomba kijana wao huyo kulinyakua jimbo hilo bila kusita.
attachment.php

hii inajulikana kwani hana kzi ya kufanya, vijana wa chadema wanaichukulia siasa kama sehemu ya riziki yao, tufanye kazi zingine kama kilimo hana jipya ni njaa tu
 
Back
Top Bottom