tarime tayari weshafanya vitu vyao...ajuza akatwa miguuu

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2
NI yowe la mjukuu wake labda ndilo lililookoa maisha ya ajuza mwenye miaka kati ya 90 na100 anayejulikana kama Sophia Makubo ambaye mtu mmoja mkatili kutoka kubiterere alimvamia nyumbani kwake na kumkata kwa panga miguu yake yote miwili.
Yowe la mjukuu huyo hata hivyo lilichelewa kuokoa miguu ya ajuza huyo ingawa mvamiaji naye alitwangwa kisawasawa na wananchi waliotikia yowe hilo la usiku na kutolewa utumbo nje ; na kufa baada ya kufikishwa hospitalini.
Taarifa zinasema ajuza huyo alikumbwa na mkasa huo mwishoni mwa wiki nyumbani kwake Ngerengere kata ya Sirari tarafa ya Inchugu wilayani Tarime Mkoani Mara.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime /Rorya Costantine Massawe alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu na ajuza huyo amelazwa katika Hospitali ya Wilaya Tarime.
 
Wamefanya makosa kumuua huyo, wangemkata miguu na yeye aonje utamu wa kutokuwa na miguu.

Masikini bibi wa watu aanze kujifunza kutembea upya bila miguu katika umri huo alionao
 
Back
Top Bottom