buffalo44
JF-Expert Member
- May 8, 2016
- 4,298
- 10,061
Polisi Nyamongo wamekuwa wakiwapiga na kuwaua raia wa kawaida kisa wameingia mgodin wakati wako nje ya eneo la mgodi.
Juzi juzi walimpiga risasi tatu mwananchi wa Nyamongo akiwa mgodini wakati walikuwa na uwezo wa kumkamata. Je, hiyo ni nzuri kumuua mtu katika nchi yake?
Kwa kweli watu wa Nyamongo wanachukia polisi kuliko mwanajeshi hadi washajilipiza kisasi vibaya hadi polisi wana gari la maji ya kuwasha na vikosi vyao sasa ni FFU tu.
Pia polisi walishawahi kumkaba shingo na kumuua kijana mmoja kisa anacheza pool. Je, hata wewe unaona ni sawa polisi kutendea raia hivyo?

Watu kadhaa wakiwemo wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika kituo cha afya cha Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara wamejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi za moto wakati askari wa jeshi la polisi wakipambana na baadhi ya wakazi wa mji huo walikuwa wakiwazuia polisi kuchukua mwili wa kijana mmoja anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi.
Tukio hilo ambalo limesababisha wagonjwa watatu ambao wamelazwa katika kituo hicho cha afya maarufu kama hospitali ya Sungusungu kujeruhiwa vibaya kwa kipigwa risasi, imeelezwa na baadhi ya viongozi wa vijiji katika eneo hilo kuwa askari polisi walianza kurusha risasi baada ya kutofautiana na familia katika kuchukua mwili wa kijana huyo Jackison Mwita.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mh John Heche ambaye ametembelea mji wa Nyamongo kufuatia tukio hilo, ameonesha kusikitishwa kwa askari polisi hao kuua wananchi kwa risasi kisha kusababisha vurugu hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu mkubwa katika kituo hicho cha afya.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Bw Gloriuos Luoga ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Tarime amesema baada serikali kupokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa jopo la madaktari, serikali itaunda tume ili kujua kiini cha tukio hilo.
Chanzo: ITV