Kuchasoni Kuchawangu
JF-Expert Member
- Aug 21, 2012
- 623
- 378
Kama matumizi yako kwa mwezi yanazidi unit 75 unatakiwa kuwa tariff 1, unit ambazo zinazodi unalipia Tsh 350 kwa unit.
Andika barua ufike ofisi ya TANESCO uliyokaribu nayo ukiomba kubadilishiwa Tariff.
Unaweza kujieidhisha kwa kuangalia kwenye risiti yako ya kununulia umeme inaonesha tariff uliyopo.
Pia unapounganishiwa umeme automatic unakuwa Tariff 1, Tariff 4 unaenda baada ya kuwa umeomba ndio unapelekwa.
Nafikiri ulishawahi kuomba kubadilishiwa Tariff? Kama bado angalia upo Tariff gani kwanza.
Mita ikiwa mpya pale wanapokufungia wanakukopesha units kadhaa ili uanzie. Sasa unapoenda kununua mara ya kwanza unalipa deni na kuendelea kununua umeme kama kawaida. Nahisi hiyo hela ni kwa ajili ya kulipia zile unit za mwanzo na wewe kupata umeme, baada ya hapo utanunua tu utakavyo
Namaanisha kwamba; mimi na wewe tumefungiwa mita mpya,halafu tumekopeshwa 50 units kila mmoja maana hawatoi zaidi au chini ya hapo.Lakini units zikiisha,tunalipa gharama tofauti.Hii inatokana na nini mkuu wakati tumekopeshwa units sawa?
Hiyo hutokea ikiwa mita yako ya zamani ilikuwa Deni tu na sio vinhinevyo
Namaanisha kwamba; mimi na wewe tumefungiwa mita mpya,halafu tumekopeshwa 50 units kila mmoja maana hawatoi zaidi au chini ya hapo.Lakini units zikiisha,tunalipa gharama tofauti.Hii inatokana na nini mkuu wakati tumekopeshwa units sawa?
Baada ya kupitia michango ya wadau hasa ufafanuzi wa hawa ndugu zetu wa ofisi ya uhusiano Tanesco nimegundua kwamba kumbe ni rahisi sana kujua kiasi cha units za umeme utakazopata kwa fedha uliyonayo. Kwamba unatakiwa kujua vitu vitatu ambavyo ni: (1) Kiasi cha pesa utakachotumia kununua umeme, (2) service charges kwa mwezi pamoja na 22% (yaani 18% VAT, 1%EWURA, 3%REA) (3) bei ya unit pamoja na 22% (kwa mchanganuo niliouonyesha hapo katika namba 2. Mfano kama wewe uko katika Tariff 1 ukitaka kununua umeme formula yake ni hivi: Fedha uliyonayo toa service charge kwa mwezi na 22% yake ambayo ni 5,520+1,114.4=6,734.4. Kiasi kinachobakia gawa kwa bei ya unit ukiongeza na 22% yake ambayo ni 298+65.56=363.56. Kwa hiyo kama una shs. 100,000 utatoa 6,734.4 ambayo ni jumla ya service charge kwa mwezi na kubakiwa na 93,265.6. Hicho kiasi kilichobaki utagawa kwa bei ya unit 363.56 na hivyo utapata unit 256.53. Kama nimechemsha basi wadau mtanisahihisha.
kumbuka unit apte hizo hutamaliza nazo mweziKwa hiyo kama una shs. 100,000 utatoa 6,734.4 ambayo ni jumla ya service charge kwa mwezi na kubakiwa na 93,265.6. Hicho kiasi kilichobaki utagawa kwa bei ya unit 363.56 na hivyo utapata unit 256.53. Kama nimechemsha basi wadau mtanisahihisha.
Ndiyo Mkuu. Hiyo kwa vile inajieleza kabisa kwamba ni monthly service charges inabidi kuzilipa tu hata kama unit zako utakuwa haujazimaliza ndani ya mwezi ulionunua hizo unit. Na hizo gharama zingine za 22%VAT ni wazi zitakatwa kwenye unit utakazonunua. Hivyo ndivyo mimi nilivyoelewa na ninaamini hivyo.kumbuka unit apte hizo hutamaliza nazo mwezi
mwezi ynaofuata ujue una Deni la Service charge ya 6.734/=
sijui km na gharama nyingine watazipiga
ukweli Tanesco wanatuumiza kwani Eanzania haikutakiwa iwe na umeme wa juu hivyo
Mtu yeyote akifungiwa meter hukopeshwa unit 50 na siku ukienda Tanesco hutakiwa kuzilipia sh 18,178 hii in gharana ya 363.56 kwa kila unit na service charge ya 6,734.40 .
Jumla ya gharama za kulipia unit 50 na service charge ni 24,912.40. Kwa mtu aliyefungiwa mfano mwezi wa 11 na kwenda kulipia mwezi wa 12, lakini mtu aliyefungiwa mwezi wa 11 akaenda kulipa mwezi huo huo halipi service charge na gharama zake ni 18178 tuu
Mtu yeyote akifungiwa meter hukopeshwa unit 50 na siku ukienda Tanesco hutakiwa kuzilipia sh 18,178 hii in gharana ya 363.56 kwa kila unit na service charge ya 6,734.40 .
Jumla ya gharama za kulipia unit 50 na service charge ni 24,912.40. Kwa mtu aliyefungiwa mfano mwezi wa 11 na kwenda kulipia mwezi wa 12, lakini mtu aliyefungiwa mwezi wa 11 akaenda kulipa mwezi huo huo halipi service charge na gharama zake ni 18178 tuu
Mkuu KOLEBA shukrani nyingi zikufikie hapo ulipo, HapaKaziTu.
Nakuomba unielimishe kuhusu swala la Voltage ndogo kwenye Cutout.
Kwenye Cutout umeme ukipimwa unasoma Volt 170 hadi 180 tu, badala ya kusoma Volt 220 hadi 240 ambazo ndiyo voltage za kawaida kwa mfumo wa umeme wa kiTanzania.
Hata kwenye sockets za ndani ya nyumba umeme ni mdogo, yaani hauzidi Volt 180. Tatizo hili linasababisha hata Friji isifanye kazi vizuri.
Kwa taarifa za vijiweni, nimeambiwa eti tatizo ni Transformer itakuwa ina uwezo mdogo kuhudumia wateja wote waliopo maeneo kama yangu yanayopata umeme kutoka kwenye Transformer hiyo.
Je, nifanye nini au nichukue hatua gani ili umeme ufikie kiwango cha kawaida cha Volt 220 adi 240 ?????
Asante kwa msaada wako mkuu. Ndiyo maana nimeshakuwa addicted na JF.