Asante sana kwa swali, Kuna tariff T1 ambayo ni kwa ajiri ya wateja wa kawaida (Normal use category) hawa ni wateja wanao tumia umeme kuanzia unit 0 - na kuendelea haina mwisho. Gharama ya umeme kwa wateja hawa ni Tsh. 298 kwa Unit na wanalipia service charge 5520+ 22% ( 22% ni VAT = 18, EWURA - 1% na REA-3%)
Tariff 4 ni kwa ajiri ya low usage customers, hawa matumizi yao kwa mwezi kuanzia unit 0-75. Gharama ya umeme ni Tsh 100 kwa unit bila service charge. Ukiwa upo tariff 4 ukatumia unit zaidi ya 75 zile unit zilizozidi utalipia Tsh 350 + 22% ya VAT.
Shurani sana wadau Koleba na wengineo tungeomba Charges kwa T2 na T3 kwa unit mana sijaona jibu hili Asante
mimi nalia na tanesco magomeni, yaani hapo prof.muhongo timua timua au wahamishe wapeleke kijijini kigoma huko baadhi ya wafanyakazi wa hapo, watu tumepeleka tatizo but hadi leo wanaleta uzushi uzushi, ikiwezekana wapige chini.
Mkuu Nando ni pm namba yako tuongee zaidi utaweza kusaidiwa.
Ila kwa kweli miye bado napinga kuwaunganisha wateja wanaotumia chini ya unit 500 kwa mwezi kwa hali hii ya umeme tuliyo kuwa nayo, Ni kujibebesha mzigo mzito mwenyewe. Kwanini usiwe na chanzo chako mwenyewe? Gharama utakayo tumia kuweka vifaa vya umeme jua haifiki kiasi unachokamuliwa na Tanesco kwa mwaka. Ukifungua macho utaliona hili 😎Asante sana kwa swali, Kuna tariff T1 ambayo ni kwa ajiri ya wateja wa kawaida (Normal use category) hawa ni wateja wanao tumia umeme kuanzia unit 0 - na kuendelea haina mwisho. Gharama ya umeme kwa wateja hawa ni Tsh. 298 kwa Unit na wanalipia service charge 5520+ 22% ( 22% ni VAT = 18, EWURA - 1% na REA-3%)
Tariff 4 ni kwa ajiri ya low usage customers, hawa matumizi yao kwa mwezi kuanzia unit 0-75. Gharama ya umeme ni Tsh 100 kwa unit bila service charge. Ukiwa upo tariff 4 ukatumia unit zaidi ya 75 zile unit zilizozidi utalipia Tsh 350 + 22% ya VAT.
Mkuu Koleba na wengine wenye ufahamu;
Juzi juzi hapa nilinunua units kadhaa za umeme wa Luku. Nilipotaka kuingiza namba husika kwenye mita ni namba mbili tu za mwanzo zilizokubali kuingia (inakuwa ina beep) lakini namba zilizofuatia ziligoma kabisa. Nilirudia mara nyingi bila mafanikio. Je ni sababu zipi zinaweza kusababisha namba zigome kuingia au ni mita ime jam? Na kama mita ni mbovu na inatakiwa kubadilishwa mimi mteja nitatakiwa kuilipia hiyo mita mpya itakayofungwa?
Mh. Koleba naona kama upo jikoni kutokana na majibu yako mazuri.Nilikuwa sijui kitu. Nakugongea like za mafuriko 😎
Mkuu ww ni jembe. Tatizo langu limekwisha mkuu.Big up sana, TANESCO inahitaji vichwa kama ww mnaejua kudili na wateja. Naomba ujitambulishe kabisha Prof. Mhongo afanye kazi na ww kwani naamini unaweza kumsaidia ipasavyo. Bravoo Mkuu
Asante Mkuu, nashukuru sana. Nilikuwa na mpango wa kukupigia leo.
Nikisema mteja wangu aneenda kimoja
Mkuu jitambulishe usiwe mwoga, kamata fursa; hunijui lakini umeniudumia ipasavyo; naamini ww ukipewa ofisi utamsaidia mzee (Prof. Mhongo) kwa kasi ya ajabu, JITAMBULISHE Mkuu usiogope......
Mkuu asante, nitachukua hatua kaka
Nimeku-search kwa TIGO pesa nikutaje? Naona unaogopa.....
Hahaha hakuna tatizo kaka nipo kwa ajiri ya kuhudumia wateja
Unaitwa Henry nadhani utakuwa makao makuu huduma za wateja TANESCO. cc Prof. Mhongo; mpe kijana ofisi naona atakufaa kutuhudumia sio "Miungu watu" walijaa kwenye ofisi za TANESCO na njaa kali ya virushwa vya kiajabu ajabu.... Bravoo Henry
Unaandika barua kwa Meneja wa Tanesco ya kuomba kubadilishiwa tarrif,ukifanya ivyo utabadilishiwaAksante sana kwa muuliza swali na mtoa jibu, hii ndiyo tunayoihitaji kwa Forum hii, maana maswali yapo clere na jibu ni sahihi na kujitosheleza kwa ufupi, natumai hata majibu kuhusu utofauti wa T1,T2 na wanaotumia 11KV & 132KV utadadavua vizuri kwa faida ya wengi na general gharama zake. Na utusaidie ni taratibu zipi zitumiwe kwa mtu kuhama Tariff, maana ukienda kuunganisha umeme kwa mara ya kwanza hope unapewa T1, Sasa unajikuta matumizi ni ya kawaida so ufanyeje? Otherwise thanks mjibu maswali@ Koleba
Ahsante sana mkuu. Ni kweli kwa maelezo yako nimeweza kujua umuhimu wa service charges. Kuhusu mita yangu maelezo yake ni: CASHPOWER, Manufactured 2006, Type 10-SA018, Landis Gyrt+. Nadhani kwa maelezo hayo utaweza kujua aina ya mita hata nisipoweka namba ya mita mkuu.Unatumia aina gani ya mita? Kama huifahamu aina dondosha mita namba hapa.
Kama mita ikionekana mbovu unabadilishiwa free of charge ndio maana service charge ikawepo( nafikiri utakuwa mmoja wa watu watakao ona umuhimu wa service charge)
Ahsante sana mkuu. Ni kweli kwa maelezo yako nimeweza kujua umuhimu wa service charges. Kuhusu mita yangu maelezo yake ni: CASHPOWER, Manufactured 2006, Type 10-SA018, Landis Gyrt+. Nadhani kwa maelezo hayo utaweza kujua aina ya mita hata nisipoweka namba ya mita mkuu.
Koleba nakushukuru sana kwa majibu yako ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwangu.