Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,338
- 13,294
Ilimchukua muda mrefu sana na baada ya kuombwa na watu mbalimbali kushiriki kampeni za Baba yetu!
Baba yetu alizunguka karibu robo tatu ya jimbo lake peke yake kufanya kampeni bila ushiriki wa Mama! Watu wakahoji kwa nini Mama yetu hampigi tafu Baba yetu bila kupata majibu!
Kumbe alikuwa anatuonea huruma! Mama anamfahamu Baba vizuri sana alivyo mkurupukaji, asivyo na subira na asivyoshaurika! Mama alitaka tuelewe kuwa kuna majanga yanatunyemelea! Lakini watu hatukumuelewa tukazidisha kumshabikia!
Mama akaona hakuna namna akaamua akajiunga katika kampeni za Baba ili isije ikaonekana anamfanyia roho mbaya na kuwa asije kulaumiwa endapo atashindwa!
Sasa Baba ameshinda na matokeo yake mmeyaona: dira imepotea, hofu kila penye ajira, mikanda imebana zaidi, mambo ya wengi yanafanywa gizani, watu hawaruhusiwi kukutana, ni marufuku kumtuhumu kwa kosa la aina yo yote, vinasa sauti vimewekwa kila kona kuwanasa watakaomsema vibaya na ameweka watu wake katika sehemu zote nyeti kumlinda!
Kwa kifupi yeye ni kila kitu! Mama aliliona hilo lakini tulimpuuza na sasa tupo kikaangioni! Sasa wote tunajuta! Tutakoma ubishi na huenda tukajifunza jambo!!!