Tanzia: Naibu Waziri Ramo Makani afiwa na mama mkwe wake

kunze

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
398
469
Naibu Waziri Wa Maliasili na Utalii,Eng.Ramo Makani,amefiwa na Mama mkwe wake Jijiji Dar.
Mazishi yanafanyika Leo kwenye makaburi ya Kinondoni.
IMG_20170519_123846.jpg
IMG_20170519_124346.jpg
 

Attachments

  • IMG_-3igndy.jpg
    IMG_-3igndy.jpg
    93.4 KB · Views: 49
Yuko kimya sana Naibu, hayumo katika kundi la wale ambao hawafanyi kazi bila waandishi wa habari kuwepo hata kama anafungua choo cha shule. Pole kwa kufiwa na mzaa chema.
 
Anatuhusu nini sisi huyu mtu..
Wale tunaoletewa taarifa zao wanatuhusu?Au unataka wale wanaojifotoa mapicha na kufuatana na waandishi wa habari?.Mkuu ungepita kimya kimya inatosha.
 
Mama mkwe? Sasa mbona ume-post hapa kwani mhusika ni mwanachama wa JF au kwa sababu ni naibu waziri? Kwa hiyo wana-JF wote tukifiwa na bibi na babu zetu tu-post taarifa ya msiba hapa.
 
Jf imekuwa hovyo sana siku hizi. Matangazo mengine ya vifo haya maana kuyaleta humu.
 
Lianzishwe jukwaa la tanzia/matangazo ya vifo Ili kila mwananchi atoe tangazo lake, haijalishi nani amefariki.
 
Neno linasema, lia na wanaolia.

Mithali 10:19,
"Katika wingi wa mambo,hapakosi kuwa na maovu.
Bali yeye azuiaye midomo yake hufanya akili"
Kila mtu anafiwa. Kila siku iendayo kwa mungu mtu anafiwa. Tutalia tuu kila siku hatutafanya kazi nyingine?
Ndio maana nikasuggest liundwe jukwaa maalum la tanzia. Mtu akitaka habari za vifo aende huko jukwaani..
.
.
huku kwenye mitandao tunategemea tuone misiba ya watu maarufu, ajali, vifo vyenye utata na kadhalika.
.
.
itafika sehemu mtu atapost JIRANI YANGU KAFIWA NA PAKA WAKE. Utakuwa utani sasa!
 
Back
Top Bottom