figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,689
- 55,662
Mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania - TBC JOE BALLONZI amefariki dunia katika Hospitali ya BUGANDO mkoani MWANZA alikokuwa akipatiwa matibabu.
BALONZI ambaye alikuwa Afisa Tehama Daraja II aliugua ghafla Februari 17 mwaka huu akiwa safarini GEITA kikazi alikoenda kufunga mitambo ya redio.
Marehemu BALLONZI alipatiwa matibabu katika Hospitali ya mkoa wa GEITA na kisha kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya BUGANDO mkoani MWANZA ambapo alifariki dunia jana usiku.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania – TBC, ametuma salamu za pole kwa wafanyakazi wote wa TBC, ndugu , jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.
Bwana alitoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe, Amen.