Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,162
- 11,229
Dar es Salaam. Hakimu mkazi mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Gabriel Mirumbe (54), amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini hapa.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Isaya Arufani alisema jana kuwa Mirumbe alifariki dunia juzi asubuhi.
Alisema Mirumbe alipelekwa hospitalini hapo Jumapili usiku baada ya kuzidiwa na maradhi yaliyokuwa ambayo hakuyataja.
Hakimu huyo ambaye ni mzaliwa wa Tarime mkoani Mara, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa nyumbani kwake Mbezi Salasala.
Enzi za uhai wake, Mirumbe alifanya kazi katika Idara mbalimbali za mahakama katika mikoa ya Kigoma, Tabora na Dar es Salaam. Akiwa mkoani Dar es Salaam, Mirumbe alifanya kazi katika Mahakama Kuu, Mahakama ya Kivukoni, na ya Kinondoni.
Akiwa katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni mwaka 1999, alimhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila kwa kosa la kutoa maneno ya uchochezi.
Mpaka mauti yanamfika, alikuwa miongoni mwa mahakimu waliokuwa wakiunda jopo la kusikiliza kesi ya wizi wa Sh6 bilioni kutoka kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) inayowakabili wafanyabiashara Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza.
​Chanzo: Mwananchi