TANZIA: Great Thinker mwenzetu, Lwitiko Edward Matipa amefariki

kimpango

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2011
Posts
600
Reaction score
717
Ulikuwa kaka, Rafiki, patner, kiongozi na yote

Tarehe Ya jana 04th October 2017 ulivuta pumzi yako ya mwisho hapa duniani. Tuanakukumbuka kwa misimamo yako isiyoyumba bila kujitakia umaarufu. Ucheshi wako na ushauri wako wa namna ya kupambana na hali za maisha wewe ukiwa ni mfano wa kweli kwa vijana.

Ukarimu wako pia ulijaliwa vipaji lukuki ikiwemo kuimba na kufundisha nyimbo. Naamini pale Conerstone Church Mwembetogwa Iringa watakumis zaidi kwa hayo

Pole Familia ya Mchungaji Edward Matipa, Pole Dada Veronica James- Manager wa Agakhan Hospital Iringa kwa kuondokewa na Mumeo

Anyway kaka Tiko you have gone too soon but God has taken one of his good fuits
Tutayaaishi mema yote uliyotuachia

Mungu akulaze mahali pema alipokuandalia, Nasi twaja.
Amen
 
Attachments

  • matipa.jpg
    matipa.jpg
    9.8 KB · Views: 120
Rest In Eternal Peace. Nyuma yako mbele yetu
 
كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَما الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ مَتَاعُ الْغُرُور

(Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Qiyaamah. Na atakayeepushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu) [Al-'Imraan: 185]

Poleni wafiwa Mwenyenzi Mungu awape subira kipindi hiki kigumu.
 
Daah kaondoka mapema sana, RIP brother.
 
Mungu anatoa na mungu hutwaa jina lake na sifa zak hudumu daima
 
Ulikuwa kaka, Rafiki, patner, kiongozi na yote

Tarehe Ya jana 04th October 2017 ulivuta pumzi yako ya mwisho hapa duniani. Tuanakukumbuka kwa misimamo yako isiyoyumba bila kujitakia umaarufu. Ucheshi wako na ushauri wako wa namna ya kupambana na hali za maisha wewe ukiwa ni mfano wa kweli kwa vijana.

Ukarimu wako pia ulijaliwa vipaji lukuki ikiwemo kuimba na kufundisha nyimbo. Naamini pale Conerstone Church Mwembetogwa Iringa watakumis zaidi kwa hayo

Pole Familia ya Mchungaji Edward Matipa, Pole Dada Veronica James- Manager wa Agakhan Hospital Iringa kwa kuondokewa na Mumeo

Anyway kaka Tiko you have gone too soon but God has taken one of his good fuits
Tutayaaishi mema yote uliyotuachia

Mungu akulaze mahali pema alipokuandalia, Nasi twaja.
Amen
Alikuwa anatumia jina gani humu?
 
Back
Top Bottom