TANZIA: Aliyewahi kuwa Rais wa pili wa Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe afariki dunia

Mkuu
Chozi lanitoka hasa apo tamim anaposema mzee imetosha sisi tushajua bila shaka yalikuwa ni mambo machungu aliokuwa anasimulia mpaka msikilizaji unachomwa moyo
 
Usimsahau na Maalim Seif Sharif Hamad.. Huyu hakustahili kutenda kile alichomtendea huyu Mzee

Naona Jamaa wa Usalama wamejaa sana hapa msibani. Ukiinua simu tu utatazamwa kama umeua mtu
Mkuu..umenichekesha apo waweza bambikiziwa kesi hjapata ona maishani...usalama wanakuangalia kama umeua mtu
 
Comrade, tuvumiliane tu...haya mambo yana mipaka yake...Mzee Jumbe tumuombee apumzike mahali pema peponi...Najua nakukwaza lakini ndiyo hivyo...Not everything is for public consumption..
But there is public interest in that...utakuwepo msibani???
 
Ngoja nione kama Maalim Seif ataenda kuhani huu msiba,kweli nitajua wanafiki hawana haya.
Mzee jumbe na seif hawanashida yeyote wanajua kuwa propaganda nani alianzisha na kwa sababu gani???
wakati tukimzika rais mstaafu abdul wakil kule zanzbar nilishuhudia haya
 
Hiki kifo cha Mzee wetu Jumbe yatupasa kitupe na mawazo mapya ya kufikiria. Tusiishie tu kuongelea kifo chake.

Yatupasa Sasa na tuangalie yale aliyokuwa anaandika Mzee Mohamed Said kwenye vitabu vyake na humu pia juu ya udhalimu wa Julius Nyerere dhidi ya wapigania uhuru wenzake wa Tanganyika.

Kile Nyerere alichowafanya wale wazee kina Sykes na wengineo, ndio haya haya aliyofanyiwa Huyu Mzee Jumbe.

Kuna watu walikuwa wanampinga Mzee Mohamed Said tena kwa matusi, tena wengine wakimuita mdini. Sasa Leo kiko wapi?

Nyerere alikuwa ni dhalimu kwenye baadhi ya Mambo na alikuwa anaendesha nchi kama Huyu wa Sasa hivi alivyo/anavyoiendesha. Alikuwa hataki kuona anakosolewa au kuna watu/mtu ni maharufu kuliko yeye. Na aliamini kuwa yeye ndiye kila kitu na ana akili kuliko wote.

Lakini mwisho wa siku yote ni ubatili mtupu. Huyo Nyerere aliishia kutangulizwa mbele za haki na kijana wake aliyemuamini sana na kumpa nchi.. lakini Nyerere akafa na kumuacha Mzee Jumbe anaendelea kuishi...
 
Mbona maalim seif amekutana naye mara nyingi tu ??? Ile ilikuwa ni fitina a Nyerere na waliitambua kama alivyotambua Amani karume
Mueleze mkuu..asante umenisaidia kidogo..propaganda hii waliomzushia seif ni sawa tu na ile walomzushia ahmed salim.mahfoudh na wengne wengi
 
Unahoja nzuri sana..
Naomba tusaidiane kumpa mwalimu mohamed said atatusaidia kwa hiri..kwani ni mtu wa karibu sana na mzee wetu
 
Wapi nimesema kimeanza julikana leo?
 


Pasco mbona unapakazia , kumbe ulikuwa katoto ka shule za chekechea za CCM . hata huelewi cho chote

umeandika

Wakamshirikisha Maalim Seif aliyekuwa Waziri Kiongozi. Seif akapanda boat usiku usiku na kuzikabidhi hizo documents kwa Mwalimu

MAJIBU

Wakati huo Maalim Seif hakuwa Waziri kiongozi

Aliyekuwa Waziri Kiongozi ni Brigadia Ramadhan Haji

Swahili Time: Sikummaliza Jumbe – " Maalim Seif"


Pasco soma tu magazeti kama wenzako au nenda kapate story za Pengo na gengi lake tehtehhhhh
 
Muongo xana wewe! Udini ulitoka wapi wakati Mwl.Nyerere amefariki akiwa mpingaji mkubwa wa udini na ukabila nchi hii! Mbona huzungumzii ya marais wengine waislamu waliofuatia,ambao ndio waliohamasisha udini hata mashuleni school uniform zilibadilishwa ili ku reflect wanafunzi na dini zao! Ama hayo huyaoni.Hapa tuna discuss political issues we unaanza udini?
 
Mkuu
Chozi lanitoka hasa apo tamim anaposema mzee imetosha sisi tushajua bila shaka yalikuwa ni mambo machungu aliokuwa anasimulia mpaka msikilizaji unachomwa moyo
Escotter,
Nyakati hufungua mambo mengi.
Tuvute subira.

Marehemu Abdul Sykes alifutwa katika historia kwa zaidi
ya miaka 50.

Leo kila siku tunamtaja hapa na watu wanashangaa kusikia
kuwa hata hilo jengo ilipoanzishwa TANU alijenga baba yake.
 

Naomba ni mtetee Mkapa kwani ali i-renovate nyumba ya marehemu mzee Jumbe kwa thamani ya TSh 80,000,000.00 (Milioni themanini) wakati wa hawamu yake ya pili. Mkapa aliwajibika vema kwa huyu mzee, Ahaji Aboud Jumbe.
 
Naomba ni mtetee Mkapa kwani ali i-renovate nyumba ya marehemu mzee Jumbe kwa thamani ya TSh 80,000,000.00 (Milioni themanini) wakati wa hawamu yake ya pili. Mkapa aliwajibika vema kwa huyu mzee, Ahaji Aboud Jumbe.
Thx mkuu
Sikulijua hili
Lkn bado viongozi wengi wa TZ hata alipofariki Nyerere waliendelea kumtenga Mzee Jumbe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…