TANZIA: Aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Philemon Ndesamburo(CHADEMA) aaga dunia

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Taarifa ambazo tumezipata za uhakika muda huu kutoka Mkoani Kilimanjaro aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mhe Ndesamburo amefariki muda mfupi uliopita.

Taarifa zaidi zitatolewa muda mfupi ujao.

tmp_10841-11187479_10205198331255349_1441120754_o1548244571.jpg

========UPDATES
Kwa masikitiko tunawatangazia kuwa, Mbunge Mstaafu wa Moshi Mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa kilimanjaro, Mhe.Pilemon Ndessamburo amefariki Dunia mapema hii leo.

Katibu wa kanda ya Kaskazini
Amani Golugwa
======

IMG_7262.JPG

Mzee Philemon Kiwelu Ndesamburo alizaliwa February 19, 1935. Alikuwa mwanasiasa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) pia kufadhili mambo mengi kupitia chama hicho.

Mwaka 2000 alifanikiwa kuchaguliwa na wananchi wa Moshi mjini kuwa mbunge wao mpaka mwaka 2015 alipoamua kwa ridhaa yake kutogombea tena jimbo hilo.

REJEA:
- Historia ya mzee Philemon Ndesamburo, aliyekuwa mbunge wa Moshi mjini

- Makala ya mwisho ya Hayati Dkt Philemon Ndesamburo aliyoiandika akimshauri Rais Magufuli
 
Uwiiiiiiiii Ndesamburo jamani!
Huyu baba ndiye aliyenifanya niijue na kuipenda Chadema kupitia jimbo nililokulia la Moshi mjini enzi zile mwaka 2000 wanagombea na Mama Minde.
R.I.P baba
Umekufa na roho yako nzuri
 
8f3fac9806d308619ee9929da43cc7b8.jpg

9b200d4caee9a8b07ff9d07f67af39c2.jpg


Taarifa za awali zinadai Mbunge wa zamani wa Jimbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Mzee Ndesamburo amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Aidha, taarifa zinabainisha marehemu amefia KCMC 'Emergency Room' alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo (heart attack).
 
Back
Top Bottom