Kama ndiyo ameanza kutekeleza ahadi zake alizozitoa kwenye kampeni za uchanguzi vyema. Hata hivyo, inahitaji mtu mzalendo na jasiri kutoa amri za chunguzi kubwa kama hizo. Hata hivyo, nahofia kama mfumo wa sheria nchini Zambia ni imara kiasi kwamba, wale wote watakaokutwa na hatia kwenye uchunguzi wanaweza kufikishwa mahakamani na hatimaye kupewa hukumu stahiri. Vinginevyo, vyama vya siasa kama CCM kwa mfano hapa kwetu, wamekuwa wadhaifu hadi kutengeneza mfumo wa kisheria imara ili kupigana vita ya ufisadi kistaarabu na kwa uwazi. Mathalani, huyo mtu anayeitwa DPP ni hatari sana katika mashauri mengi yanayohusiana na ufisadi.
Haiwezekani kumekuwa na matukio ya kifisadi kupitia DOWANS, Green Finance, Meremeta, Kagoda Agriculture, EPA, Richmond, na mengine lakini eti hata mtu mmoja maarufu kutoka kundi la wanaoeleweka kuhusika hawajawahi kufikishwa kushitakiwa, ondoa kukamatwa hata tu kufikishwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Mzee Sata ni mmoja wa waafrika wazalendo tunaowahitaji kwa nguvu zote barani mwetu. Tanzania pia tunahitaji sana mtu atakayeweza kuvunja bodi nyingi za mashirika ya umma na kuagiza chunguzi kufanyika kulingana mwenendo wa utendaji wake kuwa wa wizi wizi tu.
Tunapokuwa tunajiandaa kuelekea uchaguzi wa 2012, tunahitaji kuweka misingi itakayoweza kutupa mtu huyo adimu kumpata kutokana na chaguzi zenye kufuata sheria na haki. Kubwa tuendelee kumuomba MUNGU na mwisho wa siku hakika Sata wa Tanzania na ikiwezekana awe imara zaidi atapatikana.