Tanzanians need a leader who can do like president Sata in Zambia.....read this article please!!!

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,281
3,243
Watanzania twahitaji maamuzi ya haraka ili kupambana na udhalimu wa rushwa na ufisadi katika nchi yetu kama anavyofanya sasa rais Sata kule Zambia kwa hatua yake ya mara moja kuchunguza mikataba yote tata iliyoingiwa na rais Banda aliyemshinda kwenye uchaguzi uliofanyika majuzi tu.Hatua mojawapo ni kukatiza mara moja uuzaji wa madini ya shaba nje ya zambia bila kibali cha benki kuu yao.Watanzania tuna mengi yakujifunza toka zambia kwa sasa.....ebu usome hii article(attached).......
 

Attachments

  • Zambia.doc
    77 KB · Views: 79
Ingawa muda mwingi umepita tungeanza na NBC. Iliuzwa kwa bei ya kutupwa.
 
Kama ndiyo ameanza kutekeleza ahadi zake alizozitoa kwenye kampeni za uchanguzi vyema. Hata hivyo, inahitaji mtu mzalendo na jasiri kutoa amri za chunguzi kubwa kama hizo. Hata hivyo, nahofia kama mfumo wa sheria nchini Zambia ni imara kiasi kwamba, wale wote watakaokutwa na hatia kwenye uchunguzi wanaweza kufikishwa mahakamani na hatimaye kupewa hukumu stahiri. Vinginevyo, vyama vya siasa kama CCM kwa mfano hapa kwetu, wamekuwa wadhaifu hadi kutengeneza mfumo wa kisheria imara ili kupigana vita ya ufisadi kistaarabu na kwa uwazi. Mathalani, huyo mtu anayeitwa DPP ni hatari sana katika mashauri mengi yanayohusiana na ufisadi.

Haiwezekani kumekuwa na matukio ya kifisadi kupitia DOWANS, Green Finance, Meremeta, Kagoda Agriculture, EPA, Richmond, na mengine lakini eti hata mtu mmoja maarufu kutoka kundi la wanaoeleweka kuhusika hawajawahi kufikishwa kushitakiwa, ondoa kukamatwa hata tu kufikishwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Mzee Sata ni mmoja wa waafrika wazalendo tunaowahitaji kwa nguvu zote barani mwetu. Tanzania pia tunahitaji sana mtu atakayeweza kuvunja bodi nyingi za mashirika ya umma na kuagiza chunguzi kufanyika kulingana mwenendo wa utendaji wake kuwa wa wizi wizi tu.

Tunapokuwa tunajiandaa kuelekea uchaguzi wa 2012, tunahitaji kuweka misingi itakayoweza kutupa mtu huyo adimu kumpata kutokana na chaguzi zenye kufuata sheria na haki. Kubwa tuendelee kumuomba MUNGU na mwisho wa siku hakika Sata wa Tanzania na ikiwezekana awe imara zaidi atapatikana.
 
Isiwe ni nguvu ya soda.

Huyo Sata anajulikana kwa jina la 'King Cobra' hajawahi kushindwa jambo.
Jana alimpa waziri wake wa Sheria siku 30 za kuchunguza namna kampuni ya Zamtel ilivyo uzwa na kiasi cha pesa kilicholipwa, thamani ya mali wakati wa kuuzwa, namna zilivyotumika. Pia uchunguzi huo uende sambamba na uuzaji wa bank ya financial.
.
 
Excellent move from people's president. Haya mambo ya rais wa nchi kuanza kazi na kauli kama "mwacheni mzee apumzike" zinaonesha jinsi kusivyokuwa na dhamira ya kweli ya kupambana na kiini cha tatizo. Congrats President Sata! Usibakize jiwe lisilofunuliwa au kugeuzwa; lazima mali ya umma iheshimiwe na wote bila kujali hadhi au cheo cha mtu na kila mmoja lazima abebe furushi lake mwenyewe kwa hukumu ya haki na kuzingatia sheria.

Kama mtu hakuwa fisadi au hakuwa na uchafu mwingine alioutenda nyuma ya pazia ana haja gani ya kuogopa?
 
Mapema mno kuanza kumimina sifa, siasa na madini sio rahisi hivyo watumiaji wa shaba sio wamatumbi. Hata hivyo mwanzo mzuri
 
There is seriously a leadership vacuum in Tanzania. But its been there for the past 30 yrs or so. If anyone wants proof, just take a look around the country, you will find proof. Nothing Functions in Tanzania! To the point that even when credible evidence by the SFO is given to the PCCB to take action on grand corruption, the evidence just sits there in the file, and the file is closed.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom