Nionavyo mimi kuna matatizo yafuatay katika nchi yetu.
La kwanza kabisa ni kuwa wachimbaji wakubwa wote tulionao ni makampuni ya kigeni. Kwa hiyo Tanzania inaambulia tu kile kiichoandikwa kwenye mkataba na siyo zaidi. Katika nchi kama Afrika ya Kusini au Australia makampuni makubwa ya uchimbaji madini ni ya nchi hizo. Kwa hiyo faida inayopatikana inabakia nchini. Ghana wao wana hisa kwenye makampuni yanayochimba nchini mwao. Sisi hapa kwetu haijawezekana hata kidogo. Sielewi ni kwa nini.
Mrahaba wa 3% unatumika nchi nyingi sana duniani. Sisi tuwatoa misamaha ya kodi ambayo imekuja kutuumiza. Baada ya mikataba kuandikwa basi makampuni haya hufuata kama mikataba inavyosema.
Mara nyingi nasikia watu wakisema ati kuna ndege zinaruka kutoka nchini na kwenda nje ya nchi na madini bila sisi kujua kuwa wanatuibia. Hilo ni gumu sana kufanyika. Tunasema hivyo kwa sabau hatujui kabisa jinsi makampuni haya yanavyofanya kazi. Wamiliki wa makampuni haya ni watu wengi wenye hisa kutoka sehemu nyingi duniani. Mameneja wakiiba madini na kutorosha kutoka Tanzania licha ya kuwaiibia Watanzania wanawaibia wanahisa. Hilo hawawezi kufanya. Wanahisa wapo macho zaidi kuona kuwa kila kitu kinakwenda kama inavyotarajiwa.
Sasa hivi makampuni mengi yameanza kulipa kodi ya mapato lakini wananchi wengi hawajui hilo.Serikali nayo inashindwa kuwaeleza Watanzania kuwa makampuni yameanza kulipa kodi mbalimbali.