Tanzanian Football Clubs: So Unprofessional

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Jana club ya Simba SC imetangaza ubingwa wa VPL msimu 2019/20 hongera kwao ila pia aibu kwao kwa kuwa na brand kubwa ila iliyojaa unprofessional employees kuikuza vizuri. Simba itakuwa mfano ila club nyingi za Tanzania zinafanya haya;

1. Simba hawana mpiga picha na graphic designer
Najua hawa watu wapo ila utendaji wao wa kazi ni sawa na wao kutokuwepo, inatia aibu kuona Simba SC inapost picha zisizo na quality nzuri na kupigwa vibaya. Jana ndio walipotezwa kabisa na graphic designer wao, ile poster ya ubingwa haiendani na hadhi ya timu wanastahili zaidi ya hapo. Labda wanafanya hivi kwakuwa wabongo wengi hawafuatilii graphics ila moja ya njia nzuri kujikuza mitandaoni kama brand ni kuwa na post zenye quality na graphics kali kuvutia mashabiki au wateja, nitatoa mfano Chelsea FC inayoshiriki ligi kuu Uingereza msimu huu waliajiri freelance graphic designer kuwatengenezea poster za mechi na mashabiki walimpenda sana, kiukweli aliitendea haki kazi yake.

2. Simba hawana professional Admin
Hii shida ipo club nyingi Tanzania, nadhani wanaopewa dhamana ya kuziendesha page za club huwa hawajui admin anapaswa kupost nini na nini si cha kupost mitandaoni, page rasmi ya club sio mahala sahihi pa kupost mipasho na vijembe, nitanukuu kutoka post moja ya Simba SC "Mara tatu mfululizo, watoto watulie SIMBA ndio baba lao" such unprofessional admin will type this. Huwezi kuandika maneno ya kejeli kwenye page rasmi ya timu hapa tayari wanaunda uadui baina ya timu nyingine katika michezo Tanzania, kuchukua ubingwa isiwe njia ya kutoa kejeli kwa wapinzani wako katika ligi. EPL juzi Liverpool FC kabeba kombe na hatujaona post yenye kejeli na zaidi kocha na wachezaji wao walisikika wakipongeza wachezaji na timu pinzani.

3. Simba wanapost visivyostahili
Kupost screenshot ya CAF kisa wameretweet post ya timu ni kuwa unprofessional, hii ipo timu nyingi. Najua timu nyingi zinafanya huu upuuzi. Azam FC waliwahi kupost kuwa wamekuwa verified, Yanga SC waliwahi kupost kuwa wamepostiwa na La Liga, Simba SC jana wamepost kuonyesha retweet ya CAF. This is so unprofessional page rasmi ya club inapaswa kutoa taarifa za timu na sio kushindana mtandaoni.

4. Hili liende kwa Yanga SC
Moja ya timu inayoendeshwa kipumbavu Tanzania ni hii, inanikera kuona wanabadili logo za club nyingine tofauti na mirangi yao ya njano na kijani hasa zenye nyekundu kwenye poster zao kisa tu wana uhasimu na Simba SC basi wao wanaona kama uchawi kuvaa kitu chenye nyekundu, kubwa zaidi ni pale walipogoma kuvaa jezi zenye logo ya Vodacom. TFF walipaswa kuipa adhabu kali Yanga SC hii mentality waliyonayo ni ya kipuuzi kwenye soka la kisasa.

Kama timu kubwa zipo hivi, safari bado ni ndefu. Haya ni machache tu. Mashabiki wa hizi timu msiandike bila kuelewa ninachowasilisha.

"Unprofessional football clubs will make an unprofessional football league"
 
Unacontent kubwa sana mungu akype maisha marefu
 
Umesahau na media kama magazeti yanaandika upuuzi tu na lugha za vijiweni. Mf. Mwanaspoti utakuta font page wanaandika utumbo huu"unaambiwa huyo Morrison hagusiki, mabosi wamjaza minoti" au "Simba yaingia anga za akina Mazembe vifaa vipya kushushwa mtani achachawa". In professionalism inaanzia kwenye mamedia haya yanazijaza timu ujinga wakati bado zinajiendesha kijima.
 
Utopolo mmekosa kazi,ubingwa unawaumiza,simba ina professsional admin wa social media,siyo lazima kuiga kila kitu toka ulaya unaangalia pia hadhira yako,mbona huongelei yanga kubadili rangi za logo za timu zingine wanapopost ,simba pia inaangalia kukuza mashabiki wanapopost madongo kuna fans wanashare na wafuasi wa simba kuongezeka.

Unaposema repost ni unprofessional unajua hao walioweka walikuwa wajinga ?Simba wanaporepost vitu vya CAF inaonyesha kwamba ni kitu halisi siyo fake,hivi unafuatilia pages kama za AC Milan huwa wanapost nini?.

Page za clubs zinatumika kwa ajili ya mashabiki zao na kutoa taarifa ,uprofessional wako peleka kwenye interview za halmashauri
 
Naunga mkono hoja. Clubs nyingi bado zinaendeshwa kizamani mno, enzi za FAT kianalogia zaidi. Unakuta mchezaji wa ligi kuu au daraja la kwanza anafanya mazoezi huku kavaa jezi ya barcelona au anahojiwa na chombo cha habari huku kavaa jezi ya man city.
 
Hayo mapovu itakuwa Jana imekuuma sana mnyama kubeba ndoo, utamaduni wetu wa fasihi usiufananishe na mabeberu. Mwakani tunabeba tena.
 
Kupost vijimaneno vya vijiweni huo ni ushamba kwa page official ya timu kupost, hayo mambo wawaachie wakina Manara.

Nimewasilisha kama mambo yanayopaswa kufanyika katika taasisi kubwa kama Simba SC. Upande wangu nipo sawa na sitakuwa sawa kwa kila mtu.
 
Neutral Vodacom Premier League Fan, hata angebeba Ndanda safi tu na kama kuna sehemu wanafeli tunagonga nyundo. Hongereni Simba SC.
 
Kawasilishe na yanga pia
Kupost vijimaneno vya vijiweni huo ni ushamba kwa page official ya timu kupost, hayo mambo wawaachie wakina Manara.

Nimewasilisha kama mambo yanayopaswa kufanyika katika taasisi kubwa kama Simba SC. Upande wangu nipo sawa na sitakuwa sawa kwa kila mtu.
 
Naunga mkono hoja. Clubs nyingi bado zinaendeshwa kizamani mno, enzi za FAT kianalogia zaidi. Unakuta mchezaji wa ligi kuu au daraja la kwanza anafanya mazoezi huku kavaa jezi ya barcelona au anahojiwa na chombo cha habari huku kavaa jezi ya man city.
😂😂😂 Kuna msimu Mbao walitoa jezi majina yakawa na fonts za Premier League. Huwa najiuiliza sana hii ligi huwa inaendeshwaje kihuni-huni na ndio tunaitaa ligi kuu.
 
Nipenda sana Simba na hata club inayofanya vyema katika soka.Lakini upuuzi wa watu wachache wanohisi kujua sana kwa kujiita watoto wa mjini ndio unafanya tuone Mipira ya kibongo ni ya ajabu ajabu.

Kuna vya kujifunza
 
Forgotten umeeleza yote muhimu katika aspect ya SMM, moja ya suala jingine lenye kunisumbua ni vilabu vya ligi kuu na wachezaji kukosa profile zao na kutokuwa na social accounts, na wenye kuwa nazo hawana consistency.
 
Peleka CV yako ukapate ajira Simba Sports Club

Inaonekana unatesekaa kwelii,
 
Forgotten umeeleza yote muhimu katika aspect ya SMM, moja ya suala jingine lenye kunisumbua ni vilabu vya ligi kuu na wachezaji kukosa profile zao na kutokuwa na social accounts, na wenye kuwa nazo hawana consistency.
Kweli kabisa na vilabu vingine vina kurasa zao kabisa ila ukizitafuta unapata ukakasi kujua kama kweli ni page official ya timu, unakuta haina mpangilio na mtiririko mzuri wa machapisho.

Wachezaji nao ni muhimu sana kuwa na kurasa zao tena muhimu kuajiri na admin ambaye atakuwa ana uhakika wa kupakia taarifa za mchezaji, nadhani watanzania wengi wangekuwa wanawafatilia na hii ingewapa hata dili za kutangaza bidhaa au huduma za kampuni mbalimbali.

Tanzania tuna mfano mzuri sana; Mbwana Samatta, kiukweli post na caption zake siku hizi zinanifanya niamini kuna mtu tofauti na yeye anayeendesha page yake na kama anasimamia mwenyewe kiukweli yupo njia sahihi. Post zake za hivi karibuni nyingi zinaandikwa kwa Kiswahili fasaha na hata Instagram translator ina uwezo wa kutafsiri kwa 80% kilichoandikwa kwenda Kiingereza. Kubwa zaidi sasa ana Logo inayomtambulisha na post nyingi za matukio maalumu huwa zinafanyiwa poster design na kuwa na logo yake. Watu nyuma yake wanafanya kazi nzuri sana.
 
Kama admin kupost vijembe, mbona hata timu kubwa zinapost vijembd au kwakua vinakua kwa lugha ya malkia?
 
Aliyekwambia hizo club ni professional nani? izi club ni amature wewe ndio unaleta u profecional sehemu ambayo haupo.Wewe ndio kituko Tanzania hatuna profecional league hayo ya mitandaoni ni watu wamejiongeza.
 
Unaandika ili uonekane tu umepita hapa au ni ubishi tu ulionao?

Ninachojua mchezaji mpira professional analipwa kutokana na kazi moja tu ya kucheza soka na si vinginevyo na analipwa ili kuwa na timu muda wote atakaohitajika na hiyo ndiyo inafanya mtu kuwa professional. Simba SC inawalipa wachezaji wake kucheza soka tu na sio kingine, Simba SC ni taasisi inayoajiri Professional Football Players.

Ukisema Bongo hakuna timu professional unawakosea heshima wakina Kagere waliotoka Rwanda kuja bongo kuifata ofisi ili kufanya kazi ambayo wana taaluma nayo.
 
Back
Top Bottom