Tanzania, Zambia na China yasaini Mkataba Kufufua Reli ya TAZARA

Tanzania, Zambia na China yasaini Mkataba Kufufua Reli ya TAZARA

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
1759217650119.png

Septemba 29, 2025 Serikali ya Tanzania, Zambia na China walisaini mkataba wenye thamani ya dola bilioni 1.4 ( Takribani Trilioni 3.4 Tshs) kwa ajili ya ukarabati wa reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA), ambayo kwa miongo kadhaa imekuwa uti wa mgongo wa Biashara kati ya Afrika Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Prof. Makame Mbarawa, aliishukuru Serikali zote tatu kwa mshikamano na dhamira ya dhati ya kuhakikisha TAZARA inarejea katika ubora wake

Prof. Mbarawa pia aliwapongeza Marais watatu: Rais Xi Jinping wa China, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha hatua hiyo muhimu ya uhai mpya wa Shirika hilo la Reli

1759217726287-png.3481161

Waziri huyo alibainisha kuwa kufufuliwa kwa TAZARA kutakuwa na manufaa makubwa, yakiwemo Kuimarisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zambia na nchi nyingine wanachama wa SADC,Kupunguza gharama na muda wa usafirishaji, Kuchochea biashara ya kikanda na kuvutia wawekezaji, Kuongeza ajira na kipato kwa Wananchi, Kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia na kiuchumi kati ya Tanzania, Zambia na China

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Zambia, Mhe. Frank Tayali, alisema mkataba huo umesainiwa kwa wakati muafaka, na mara baada ya maboresho kukamilika, Reli hiyo itaimarika zaidi na kupanua wigo wa usafirishaji wa abiria na mizigo kwa nchi zinazotegemea huduma za treni

Reli ya TAZARA, iliyojengwa miaka ya 1970 kwa ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania, Zambia na China, imekuwa mhimili muhimu wa uchumi wa kikanda. Kufufuliwa kwake kunatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kukuza Biashara, Ajira na Maendeleo ya kanda nzima ya Afrika Mashariki na Kusini

Soma pia China kuendesha TAZARA kwa miaka 27, Uwekezaji wa dola bilioni 1.4 kuanza
 

Attachments

  • 1759217726287.png
    1759217726287.png
    2.2 MB · Views: 32
Ingelikua ya umeme(Electrified SGR(high speed, bullet train)), Ingeliongeza point tatu za ushawishi na ushindani kwa washindani wanaokuja kimkakati.

Na ukizingatia mchina ndio mkali wa hizi kazi...
 
Ni kama mwaka sasa nasikia china njaa ni mbaya, naona wamekuja kutafuta ajira bongo kwa mgongo wa reli, reli zenyewe wanajenga za mchongo.
 
30 September 2025
Waziri Frank Tayali na waziri Prof. Mbarawa wakiongea baada ya kusainiwa dili hilo la US$ 1.4 kukarabati reli ya TAZARA


View: https://m.youtube.com/watch?v=VbZhjNKloes

Zambia, China and Tanzania have signed the Tanzania-Zambia Railway (TAZARA) Revitalization Project Agreements after over one and half years of negotiations. The Revitalization Project will cost US$1.4 billion, of which the initial investment will be $1.1 billion, and $238 million will be re-investments...

View: https://m.youtube.com/watch?v=xNmtFkVG_hQ
 
Kama ni mchina anaweka pesa zake sio mbaya , usije ikawa ni mkopo
 
Back
Top Bottom