Tanzania yetu bado unaweza kuwa na ndoto na kufanikiwa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Ni nchi chache sana hapa duniani ambapo mtoto wa ktk familia masikini anaweza kuwa na ndoto na kuitimiza na sisi ni mojawapo, nimemsikiliza mkuu wa mkoa wa Dar yetu Makonda akisema alikotoka ni kwamba mama yake siyo msomi wala baba yake ina maana anatokea familia ya chini lkn leo hii ni mkuu wa Mkoa muhimu na tajiri klk yote nchini mwetu, hata raisi wetu Magufuli ametokea chini kabisa amejiendeleza mwenyewe kuanzia ualimu mpaka PhD leo hii ni raisi wa TanZania, mzee Mwinyi vivyo hivyo alikuwa Mwalimu tu akajiendeleza mpaka kuja kuwa raisi wa nchi hii!

Hii ni nadra sana hapa Duniani nchi nyingi sana viongozi wakubwa ni kwa wale maelite na maestablishment tu wao pmj na familia, ndugu na jamaa zao lkn kwetu bado unaweza kuwa na ndoto na haijalishi wewe ni masikini kiasi gani na ukafika mbali mkuu wa mkoa wa Dar yetu pamoja na raisi wetu ni shahidi wa hili!

Hivyo kwangu mimi hii ni sababu tosha kabisa ya kuendelea kuiamini ccm pmj na mapungufu yake yote lkn ndani ya ccm unaweza kuwa ndoto na siku moja ukaitimiza na haijalishi familia unayotoka maadamu unajituma na uko tayari kwa changamoto kama kuna yoyote atafutaye ushahidi ni raisi wetu Magufuli, mkuu wetu wa Dar na wengineo wengi tu!!
 
Utawadanganya wachache sana ila wengi wanajua ccm ina wenyewe, sasa hivi mbunge ndani ya ccm akifariki nafasi yake anapewa mtoto wake bila kujali wanachama wanaokipigania chama wa sehemu husika, tumeona kwa kina Kombani kijana katoka Dar kaja kugombea ubunge Mahenge na kurudi Dar, kina Kigoda, Kina Mgimwa, na wengine wengi tu sehemu hizo kama kina Kigoda watu walikuwa hawamkubali kabisa lakini ccm kama kawaida wakabaka mapendekezo ya wengi na kutimiza haja za wamtakao wao. ccm hii ina wenyewe na wenyewe ni wale k wakaao karibu na kina fulani kila mtu anjua Makonda ametoka kwa kushikwa mkono na nani, Mafgufuli angekuwa ndio anagombea ubunge leo wala hakuna namna angepenya amepata nafasi wakati ccm ikiwa cham kweli cha kutetea wanyonge.
 
Back
Top Bottom