Tanzania Yenye Neema ni ile itakayorekebisha sheria za kodi

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Ili Tanzania yenye neema na rehema ipate kuwa, basi ni lazima sheria za kodi zirekebishwe. Tanzania hiyo tunayotaka ni ile ya watanzania wenye purchasing power kubwa.

Kwa mimi nionavyo, Tanzania ikipunguza kodi zake hadi asilimia takribani 8% hivi, itakusanya kodi kubwa sana mara 1000 zaidi inavyokusanya leo na kwayo kumuongezea mwananchi purchasing power. Hii sheria iliyopo sahivi, yani sheria ya kodi ni sheria mbovu inayoharibu uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

Huwezi pata wawekezaji kama cooparate tax ni 30%. Huwezi pata wawekezaji kama import ya vitu ni zaidi ya 100% ya bei uliyonunulia , hii ni obvious bei ya kiwanda hicho products zake bei itakuwa juu.

Hii ndiyo maana sukari iliyozalishwa Brazil ikalipiwa huko kodi ikasafirishwa mpaka Tanzania bado inakuwa bei ya chini kulinganisha na ya mtibwa ama kagera. Tunatakiwa kuwa na mentality ya competitive.
 
Uko sahihi sana
 
Kwa Ujumla " Easy doing business " inatakiwa iboreshwe katika vipengere vyake vyote, maana yake na hoja yako inaingia hapo.
Neema ya kweli hailetwi na serikali bali Serikali inatakiwa iweke mazingira mazuri ili neema za kweli ziwe halisi kwa kila mtanzania mwenye nia njema.

Tujifunze INDIA
PM Modi asks secretaries to analyse World Bank’s Ease of Doing Business Report - Times of India
Mazingira ya kiwanda au biashara kufanikiwa Tanzania yanatakiwa kuwa bora kuliko washindani wetu. Waziri mkuu wa india alipoona hali sio nzuri kwao, kaagiza makatibu wakuu wote wa mawizara wakae waje na solution ya kudumu huku akiwaahidi wenye makampuni kuwa hali itakuwa nzuri. Hii kitu inahitaji collective decision sio wizara ya viwanda tu au TRA peke yake kama tukiamua kuwa makini inawezekana mkuu
 
Mmezoe kupiga dili tuuu lipeni kodi bhnaa hii nchi ni tajirii mpaka tunaelekea kuwa donor country.....

Lipeni kodi wacheni dili dili

If i kudu bi a TRA kamishna..... In Sizonje's voice....
 
Wanaotunga sheria za kodi wao haziwahusu "kivile"

Nafikiri zinawahusu ila nafikiri hawangalia ktk muktadha ulio sahihi zaidi. Wao nafikiri, wanafikiri wakikata bei kubwa kodi ndo wanapata fedha nyingi, no no it's wrong. Ukitaka kukamua maziwa mengi ngo'mbe wako mlishe vizuri kila siku. Hii kodi haikai vizuri ktk uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.
 
Mmezoe kupiga dili tuuu lipeni kodi bhnaa hii nchi ni tajirii mpaka tunaelekea kuwa donor country.....

Lipeni kodi wacheni dili dili

If i kudu bi a TRA kamishna..... In Sizonje's voice....

Tatizo lako siasa, sheria hizi za kodi siyo za jana wala juzi zipo siku nyingi.
Hii ndo sababu hata TTCL wana strugle kufikiri kutoza kwa bei kubwa kubwa wateja unaopata ni wachache zaidi ya potentials wengi.
 
Kwa Ujumla " Easy doing business " inatakiwa iboreshwe katika vipengere vyake vyote, maana yake na hoja yako inaingia hapo.
Neema ya kweli hailetwi na serikali bali Serikali inatakiwa iweke mazingira mazuri ili neema za kweli ziwe halisi kwa kila mtanzania mwenye nia njema.

Tujifunze INDIA
PM Modi asks secretaries to analyse World Bank’s Ease of Doing Business Report - Times of India
Mazingira ya kiwanda au biashara kufanikiwa Tanzania yanatakiwa kuwa bora kuliko washindani wetu. Waziri mkuu wa india alipoona hali sio nzuri kwao, kaagiza makatibu wakuu wote wa mawizara wakae waje na solution ya kudumu huku akiwaahidi wenye makampuni kuwa hali itakuwa nzuri. Hii kitu inahitaji collective decision sio wizara ya viwanda tu au TRA peke yake kama tukiamua kuwa makini inawezekana mkuu

Nakubaliana na wewe mia kwa mia.
Mazingira ya kufanya biashara Tanzania ni magumu yakichangiwa na kodi zisizo na maana.
 
Ili Tanzania yenye neema na rehema ipate kuwa, basi ni lazima sheria za kodi zirekebishwe. Tanzania hiyo tunayotaka ni ile ya watanzania wenye purchasing power kubwa.

Kwa mimi nionavyo, Tanzania ikipunguza kodi zake hadi asilimia takribani 8% hivi, itakusanya kodi kubwa sana mara 1000 zaidi inavyokusanya leo na kwayo kumuongezea mwananchi purchasing power. Hii sheria iliyopo sahivi, yani sheria ya kodi ni sheria mbovu inayoharibu uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.

Huwezi pata wawekezaji kama cooparate tax ni 30%. Huwezi pata wawekezaji kama import ya vitu ni zaidi ya 100% ya bei uliyonunulia , hii ni obvious bei ya kiwanda hicho products zake bei itakuwa juu.

Hii ndiyo maana sukari iliyozalishwa Brazil ikalipiwa huko kodi ikasafirishwa mpaka Tanzania bado inakuwa bei ya chini kulinganisha na ya mtibwa ama kagera. Tunatakiwa kuwa na mentality ya competitive.
Mkuu unasema corporate tax kwa Tanzania ni 30% na import tax ni kama 100%. Hii ina maana sukari inayoletwa toka Brazil inatozwa zaidi ya 100%. Kwa hiyo sukari ikiingia inatozwa 100% ikiwa ni import tax na huyo mtu akiingiza na kuiuza anatozwa 30% sasa inakuwaje hiyo sukari iwe rahisi kuliko inayozalishwa nchini ambayo haina 100% ya import tax?
 
Gharama ya uzalishaji sukari TZ ni kubwa kuliko kuzalisha Brazil +kusafirisha +kodi.
 
Tatizo lako siasa, sheria hizi za kodi siyo za jana wala juzi zipo siku nyingi.
Hii ndo sababu hata TTCL wana strugle kufikiri kutoza kwa bei kubwa kubwa wateja unaopata ni wachache zaidi ya potentials wengi.
Mkuu hujanielewa tuuuu......
 
Mkuu unasema corporate tax kwa Tanzania ni 30% na import tax ni kama 100%. Hii ina maana sukari inayoletwa toka Brazil inatozwa zaidi ya 100%. Kwa hiyo sukari ikiingia inatozwa 100% ikiwa ni import tax na huyo mtu akiingiza na kuiuza anatozwa 30% sasa inakuwaje hiyo sukari iwe rahisi kuliko inayozalishwa nchini ambayo haina 100% ya import tax?
Mazingira ya uendeshaji viwanda hapa nchini ni magumu na yenye gharama kubwa.... Achilia mbali kodi gharama za uendeshaji ni kubwa mno.....
 
Swali zuri,
Hii ndiyo maana huwa wanatafuta crisis kupata msamaha wa kodi ya imports. Bila hivyo hawa import kitu chochote. Na kama baa la njaa walikuwa wanatafuta crisis wapate msamaha wa hiyo kodi waingize chakula. Bila ujanja ujanja Tanzania ni nchi ngumu sana kwa kufanya biashara.
 
Tanzania washushe cooparate tax mpaka 8%. Hii itavutia wawekezaji waje wajenge viwanda Tanzania Dell wakija Tanzania wakatengeneza faida ya 50 Dolla bilion hata ukimkata 5% unapata dola bilion 2.5. Ukipata wawekazaji 10 wa hivyo ukawakata 5% cooparate tax unapata 25 dola bilion. Pesa unayopata kuendesha serikali nzima maana hapo ni zaidi ya mara 3 ya bajeti nzima ya Tanzania.

Kinyume chake ng'ang'ania makodi makubwa unapata zero mwekezaji na 0$. Hii ndo maana Kenya kwa namna nyingine yanatuzidi na tunashangaa, shangaa tu.

Kingine punguza import pale bandarini, mpaka 8% utapata wateja wote wa SADC na utapata bilion bilion of $$$ wala hutahitaji kwenda kubebeleza rais yoyote kwamba wafanya biashara waje wapitishe mizigo. Kinyume chake, fanya import zaidi ya 100% utavuna huto twa kuvuna na kubaki kushangaa kwanini hatuendelei.
 
Ni suala la welewa na kama huelewi kukubali ushauri.Nakubaliana na mtoa mada kuwa punguza kiasi cha kodi kisha pata wawekezaji wengi harafu u una make zaidi.ni kama duka la rejareja punguza bei kisha pata wateja wengi then mauzo makubwa mwisho faida na maendeleo zaidi kutokana na mzunguko wa biashara
 
Tanzania washushe cooparate tax mpaka 8%. Hii itavutia wawekezaji waje wajenge viwanda Tanzania Dell wakija Tanzania wakatengeneza faida ya 50 Dolla bilion hata ukimkata 5% unapata dola bilion 2.5. Ukipata wawekazaji 10 wa hivyo ukawakata 5% cooparate tax unapata 25 dola bilion. Pesa unayopata kuendesha serikali nzima maana hapo ni zaidi ya mara 3 ya bajeti nzima ya Tanzania.

Kinyume chake ng'ang'ania makodi makubwa unapata zero mwekezaji na 0$. Hii ndo maana Kenya kwa namna nyingine yanatuzidi na tunashangaa, shangaa tu.

Kingine punguza import pale bandarini, mpaka 8% utapata wateja wote wa SADC na utapata bilion bilion of $$$ wala hutahitaji kwenda kubebeleza raisa yoyote waje wapitishe mizigo. Kinyume chake, fanya import zaidi ya 100% utavuna huto twa kuvuna na kubaki kushangaa kwanini hatuendelei.
Sasa taarifa zinadokeza kwamba wataalam wapo kama maboya tu , maagizo yote anatoa mtu mmoja tu , tena ambaye hajawahi kuuza hata Mapera .
 
Tanzania washushe cooparate tax mpaka 8%. Hii itavutia wawekezaji waje wajenge viwanda Tanzania Dell wakija Tanzania wakatengeneza faida ya 50 Dolla bilion hata ukimkata 5% unapata dola bilion 2.5. Ukipata wawekazaji 10 wa hivyo ukawakata 5% cooparate tax unapata 25 dola bilion. Pesa unayopata kuendesha serikali nzima maana hapo ni zaidi ya mara 3 ya bajeti nzima ya Tanzania.

Kinyume chake ng'ang'ania makodi makubwa unapata zero mwekezaji na 0$. Hii ndo maana Kenya kwa namna nyingine yanatuzidi na tunashangaa, shangaa tu.

Kingine punguza import pale bandarini, mpaka 8% utapata wateja wote wa SADC na utapata bilion bilion of $$$ wala hutahitaji kwenda kubebeleza raisa yoyote waje wapitishe mizigo. Kinyume chake, fanya import zaidi ya 100% utavuna huto twa kuvuna na kubaki kushangaa kwanini hatuendelei.
Mkuu hivi bidhaa za DRC na nchi zingine zinatozwa kodi zikiingia bandari ya Dar?
 
Mkuu
Ni ndiyo zinapigwa kodi, sema uulizie kodi hiyo jina lake linaitwa labda jina tofauti. Lakini kodi wanalipa na ndiyo wengine kimewakimbiza pia

Tanzania: Revenue Authorities Smooth Trade With DR Congo
Tagged:

By Leonard Magomba
Dar es Salaam — Revenue authorities in Tanzania and the Democratic Republic of Congo (DRC) have teamed up to enhance a smooth flow of transit goods through the Dar es Salaam Port as well as to curb theft of goods between the two countries.

Tanzania is reported to have incurred losses amounting to over Tsh20b ($12.73m) due to practices related to dumping and compensation of goods lost in transit by the traders using Dar es Salaam Port as their gateway.

http://allafrica.com/stories/201209040975.html
 
Mazingira ya uendeshaji viwanda hapa nchini ni magumu na yenye gharama kubwa.... Achilia mbali kodi gharama za uendeshaji ni kubwa mno.....
Mkuu huenda kweli gharama za uendeshaji zipo juu na si suala la kodi pekee. Kama nchi tunatakiwa kuangalia gharama za uzalishaji kwa ujumla wake. Kuna masuala ya umeme, upatikanaji wa maji, miundombinu mbalimbali na hata masuala ya kodi. Tuangalie kwa nini bidhaa toka nje zinaingia na kutozwa kodi forodhani lakini bado zingine zinakuwa rahisi. Hivyo unaweza kuona kwamba kuna vitu vingi badala ya kodi peke yake.
 
Hayo yote mtukufu hayaoni.... Yeye anakazania watu wanapiga dili tuuu....

Kenya inakimbia sana kiuchumi coz amezinduka na kukamatia fursa!!

Dubai leo ukitaka kuwekeza kuna vivutio chungu mzima na mazingira yanayoeleweka!! Nani leo ataichagua TZ kati ya Dubai ili aje awekeze?

Mwambieni ngosha haya mambo hauahitaji kufoka foka hovyo
 
Back
Top Bottom