Tanzania yazindua mgodi

Tanzania yazindua mgodi

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake wa kwanza utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa Watanzania.

Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo.

Saumu Mwasimba amezungumza nae mchana huu na kutupa maelezo kamili kuhusu mgodi huo na hatua hiyo ya serikali. Kuskiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=179342&d=1408691837[/JFMP3]

Chanzo: DW
 
Attachments

Hii sio Tulawaka ambayo walinunua kutoka African Barrick?
 
Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa Watanzania.

Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa

wewe prof. ni msomi sana, haiwezekani miradi mikubwa kama hiyo iwe ya kutatua ajira tu. kwa hiyo nchi ina tatizo la ajira pekee? au ndo miradi ya kampeni? kuajiri watu tu hata kama hamna uzakishaji? nafurahi kusikia miradi kama hii inafunguliwa lakini you have to focus, broadly, what to address, ongezea basi kwamba mradi utaongeza pato la taifa, kupunguza matatizo ya afya, elimu, kisha ujenzi wa miradi mingine kutokana nao (multiplier effect).

ONYO: najua hapa kuna wafia serikali/chama watakuja kuharisha kama kawaida yao kwa sababu hawajui kuelewa kilichoandikwa, nawasubiri. cc MSALANI Lizaboni
 
Huo siyo mgodi mpya, ni ule ulewa Tulawaka ambao Afeican Barrick Gold wamechimba dhahabu karibu yote, ndiyo Stamico wameachiwa mapango wakombeleze mabaki. Hahahahahaa... Watanzania fungu la kukosa!
 
Huo mgodi wa tulawaka umebaki makapi huyu mulongo aache uongo wke anachimba nini hapo
 
Jk amewashika pabaya CDM kila mkitukana yeye apiga kazi excuse zinaisha na mwaka 2015 ndo huo mje kusingizia makontena ka Kura yameletwa toka Mbeya
 
Chini ya Uongozi wa S.Muhongo,Wizara ya NM inapiga hatua haraka haraka

Huo siyo mgodi mpya, ni ule ulewa Tulawaka ambao African Barrick Gold wamechimba dhahabu karibu yote, ndiyo Stamico wameachiwa mapango wakombeleze mabaki. Hahahahahaa... Watanzania fungu la kukosa!
haya sasa. profesa upoooo?? wenye nchi wameshtukia...
 
kama hujui kitu uliza, STAMICO hawachimbi pale Barrick alikuwa anachimba wameanza eneo linguine jipya kabisa

Eneo lipi ambalo stamico wanachimba au wameanzisha huo mgodi fafanua
 
Tatizo la laana ya hii nchi mradi kama huu inatakiwa tuulee usaidie nchi na tuache kupiga mayowe ya kusema ooh wamechukua kila kitu wao tuu wazungu, utashangaa akipewa mtu kazi hapo ndio hafiki kazini kisingizio mama yangu, mtoto, msibaa ooh ili alale tu lakini alipwe,!!!! ni laana ya Afrika hatujitumi kazi yetu kupiga mayowe na kukosoa kwa maneno vitendo hakuna!!!
 
Ndo wenyewe,mzungu ameshindwa kuuendesha wabongo tutaweza kweli ngoja tujaribu.

Mkuu huo mgodi dhahabu ya maana wazungu walishamaliza sasa tunaenda kupoteza hata kidogo tulichokuwa nacho kwa kutafuta dhahabu ambayo haipo? Yaani tunaenda kucheza na vifusi tu! Kama uwezo Wa kusimamia mgodi tunao kwa nini tusitafute mgodi mpya tujenge wenyewe?
 
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi mgodi wake wa kwanza utakaowaajiri wafanyakazi wazawa tu kuanzia ngazi za uongozi hadi chini.

Hatua hiyo imechukuliwa na serikali kama juhudi za kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa Watanzania.

Aidha waziri wa nishati na madini nchini humo Sospeter Muhongo amesema mgodi huo wa dhahabu wa Biharamulo utafuatiwa na mingine kadhaa itakayotowa pia nafasi za ajira kwa wazawa ingawa amesisitiza Tanzania haina nia ya kuwafukuza wageni wanaosimamia migodi mingine ya nchi hiyo.

Saumu Mwasimba amezungumza nae mchana huu na kutupa maelezo kamili kuhusu mgodi huo na hatua hiyo ya serikali. Kuskiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=179342&d=1408691837[/JFMP3]

Chanzo: DW

Duh! siku zote nilidhani migodi imemilikiwa na kuwanufaisha Watanzania, noma sana aisei.
kadoda11 Bulldog Geza Ulole
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom