Tanzania yatimiza malengo. Sasa rasmi ni nchi ya ahadi

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Wanabodi, Maandiko ya historia kwenye vitabu mbalimbali yanaonyesha kuna kizazi hapa duniani cha wanaisrael kiliahidiwa nchi ya ahadi na ahadi ikatimizwa, Ingawa safari kuelekea nchi ya ahadi ilikuwa na misukosuko kwa wanaisrael wachache walifika nchi ya ahadi.

Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa CCM kuamua kimabavu kuwaweka viongozi wa mitaa ili watuongoze kinguvu imetimia, Hali hii ilisubiriwa na wengi baada ya uchaguzi wa 2015 sasa imetimia

Wananchi Tanzania sasa tegemeeni neema na maendeleo makubwa kuelekea chama kimoja cha CCM.

Dodoma Itakuwa kama New York City, Hili jiji ifikapo 2020 Itakuwa sehemu ya kuigizia filamu na kutoa series au episode mbalimbali.

Wabunge wa Chama kimoja CCM ifikapo 2020 watapigania kila Mtanzania apokee pesa taslimu bure bila kufanya kazi yeyote ile

Hakuna haja ya kufanya kazi kwani serikali ya chama kimoja itatoa chakula, mavazi, mboga na matunda kwa kila Mtanzania, Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kufurahia uchaguzi ambao tutakuwa na chama kimoja

Wabunge wa chama kimoja ndio Think Tank wa Taifa kwani ifikapo 2020 watapata idea na mawazo mapya ya kuendesha nchi. Hapo awali akili zao zilichoshwa na hali ya ushindani katika kugombea hivyo kuwa na mawazo mafupi

Nchi ya ahadi iliyohubiriwa tangu uhuru sasa inakwenda kutimia, kutakuwa na shule za serikali tu ifikapo 2020

Biashara zitafanywa na serikali tu ifikapo 2020.

Makampuni mengi binafsi yatahodhiwa na serikali tu kwa kupokwa toka kwa watu binafsi

Tunapounga mkono juhudi pia tujiandae kisaikolojia kuporwa mali zetu na ni nani atakayekusemea?
 
Niseme kwa imani yangu Mungu anamakusudi yake kumwacha shetani ajiiinue.
Iweje rais TEC kiongozi Wakatoliki, wazee wenye hekima wapo kimya na kuamua kusifia, hakika karibia tufike Kaanani.
 
Hakika umenena na siku zaja CCM akili zitawaijia ndipo watakapoelewa kwa wapinzani sio adui yao wataelewa wakiwa wameshachelewa.
 
CCM ni sawa na kenge hadi yawakute ndo uelewa akimauliza kuubomoa upinzani lazima aibomoe CCM aunde mfumo wake hapo ndipo CCM watakapounga dhidi ya adui wa haki. Ngumu kuelewa kwa sasa lakini siku zaja si mbali
 
Mithali 22:7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye..

Maendeleo yatokanayo na mikopo? Ndiyo unayoyalenga? Mabeberu wanawakopesha bila masharti? Au Yale mnayaita masharti nafuu? Mnaiandaa nchi kuwa watumwa kwa ....
 
Kila siku anakopa, huku anatamba kuwa tunatumia pesa za ndani!
Haijwahi kutokea duniani kuwa na kiongozi muongo hivi.
 
Back
Top Bottom