Tanzania yatajwa kuongoza kwa kukandamiza upinzani Afrika

Targaryen

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
675
640
Ripoti ya Amnesty International

Kwa mujibu wa shirika la Amnesty International Kenya na Tanzania zimetajwa katika jumla ya nchi za kiafrika ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuwakandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea.
Shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International, limesema mwaka 2016/17 uligubikwa na wimbi la uvunjifu wa haki za binadamu.

Pia limeeleza kuwa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari, kwa mfululizo, wameendelea kukabiliwa na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa haki ya uhuru wa kujielezea ilikabiliwa na mmomonyoko mkubwa pamoja na wimbi jipya la vitisho kutoka katika vyombo vya dola.

Kumekuwa na jaribio la kukandamiza wapinzani na kunyongesha uhuru wa kujielezea vilivyo jitokeza katika bara zima la Afrika, imesema ripoti hiyo.

Nchi nyingine zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo na kuhusishwa na uvunjifu huo wa haki za binadamu ni pamoja na Botswana, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d’Ivoire, Gambia,Mauritania, Nigeria, Somalia, South Sudan, Sudan, Togo and Zambia.

Ripoti imesema hayo ni kati ya zaidi ya matukio 177 ya watu binafsi waliouwawa kinyume cha sheria, wakati wakiwa mikononi mwa vyombo vya usalama kwa mwaka mzima (2016/17).

Nchi nyingine hizo 14 ziliorodheshwa ni kati ya zile zinazoongoza katika kukandamiza uhuru wa kujielezea na pia ukamataji wa kiholela na kuwaweka kizuizini wanachama wa vyama vya upinzani na makundi mengine.

Katika ripoti hiyo ya Amnesty International matukio mengi yameshuhudiwa katika maeneo ya pwani, na vitendo hivyo vya uvunjaji wa haki za binadamu vimekuwa vikitekelezwa kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na mashambulizi ya kundi la kigaidi la al-Shabaab.

“Kwa mujibu wa Haki Afrika, kikundi cha haki za binadamu, kulikuwa na mauaji 78 kinyume cha sheria na kutoweka kwa watu bila ya taarifa yoyote katika kaunti ya Mombasa katika miezi 8 ya kwanza ya 2016.
 
TANZANIA ITAMETAJWA KUONGOZA KWA KUKANDAMIZA UPINZANI AFRIKA
Duuuh.....unataka kutuambia nini hasa kutokana na heading yako?????......maana hamna mahali AMNESTY wamesema TANZANIA imeongoza AFRIKA......bali ni miongoni mwa nchi
 
Mbunge LijiaLikali kafungwa jela miezi 6 eti kwa kosa la 'kuwapiga' maaskari wenye silaha za moto wakati yeye akiwa hana hata kirungu!

Mbunge Lema huu ni mwezi wa 4 yupo mahabusu kwa tuhuma ya kosa linalodhaminika!

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew kafungwa jela miezi 8 eti kwa kosa la kufanya mkutano wa kisiasa bila kupewa idhini na Polisi!

Hakika tathmini hiyo ya Amnesty International inaweza kuwa na ukweli wa asilimia kubwa kuwa nchi yetu inaweza kuwa ndiyo kwa sasa ikawa ndiyo kinara wa kukandamiza upinzani kuliko nchi yoyote barani Afrika!
 
Hao Amnest International ni wanafiki!

Wapinzani wa Tanzania baada ya Kumchoka Jk wakasema kwa Hali iliyokuwa imefikia kwa Nchi kukosa nidhamu tulimhitaji Dikteta
 
Nadhani tunaongoza by far, na tutazidi kupaa kwa sababu tuna wakimbiaji maarufu wa marathon
 
TANZANIA ITAMETAJWA KUONGOZA KWA KUKANDAMIZA UPINZANI AFRIKA
Duuuh.....unataka kutuambia nini hasa kutokana na heading yako?????......maana hamna mahali AMNESTY wamesema TANZANIA imeongoza AFRIKA......bali ni miongoni mwa nchi
Kwani ni uongo??
Ni nchi gani hapa Africa yenye mambo ya kipuuzi puuzi dhidi ya wapinzan kama Tz?
 
EU na USA wamekataa kuchangia Budget

Kati ya Misaada waliyo ahidi ni 30% tu wametoa..

Tanzania ni nchi masikini na bado tunahitaji misaada...msidanganyike na propaganda

-Ndio maana Pesa zilizochangwa za waathirika Tetemeko...Zimechukiliwa na Serikali

--ndio maana hawana pesa za kutoa mikopo kwa wanafunzi

---ndio maana wanachukua pesa za mifuko ya jamii kama PPF, NSSF mpaka ule wa bima ya afya

----ndio maana dawa hospitalini hakuna (DENI LA MSD bado lipo)

-----ndio maana Waalimu wanadai madeni

------Ndio Maana budget ya Serikali imekwama (Ile trillioni 29 haitafika)

Shillingi imeanguka thamani na mfumuko wa bei

Maamuzi wa wanasiasa kuleta sheria kandamizi ili wabaki madarakani kwa Hila ndo sababu....Bora wananchi waumie kuliko wao kutoka madarakani

Sheria ya mitandao

Sheria ya vyombo vya habari

Uchaguzi Znz

Mikutano ya hadhara kuzuiwa
 
Back
Top Bottom