Tanzania yashika nafasi ya pili kwenye matumizi ya Teknolojia Barani Afrika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
tech.jpg

Tanzania imeshika nafasi ya pili kati ya nchi arobaini na nne zinazopiga hatua kwenye matumizi ya teknolojia katika shughuli za maendeleo barani Afrika hali iliyotokana na watanzania kupata mwamko mkubwa wa kutumia teknolojia katika shughuli za maendeleo ya kila siku.

Kauli hiyo imesemwa na watalaam wa masuala ya sayansi na teknolojia katika uzinduzi wa ripoti ya matumizi ya teknoljia katika shughuli za maendeleo iliyofanyika kwenye taasisi ya sayansi na teknolojia ya Nelson Mandela ambapo katika ripoti iliyo zinduliwa nchini Senegal inaonesha Tanzania imeshika nafasi ya pili ikitanguliwa na nchi ya Moroco.

Mwenyekiti wa Chama cha Hisabati Tanzania Emmanuel Kisongo,amesema tafiti pia zinaonyesha kuwa bara la Afrika bado liko nyuma katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu katika kukuza uchumi wa nchi pamoja na watu wake ukilinganisha na nchi zilizoendelea.

Mratibu wa Mradi unaosimamia tafiti hizo kutoka shirika la African Capasity Building Foundation (ACBF) la nchini Zimbabwe,Dkt.Michael Haule amesema Tanzania kupitia taasisi ya Nelson Mandela imeweza kunufaika na mradi huo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.

Chanzo: ITV
 
Safari bado ndefu sana, Nchi zingine Africa zilishapita huko siku nyingi.... sisi ndo tunakoelekea huko, hata hivyo nafikiri ni kwa sababu watanzania wengi hatuna elimu ya kutosha kuhusu masuala ya teknologia!!!!!
 
Nimekuja mbio nikidhani tumeshika nafasi ya Pili kwenye kutumia teknologia ya kijasusi kama ile aliyotumia mwana koromije mmoja kusepa na flash yenye kipindi chake bila kuacha nyayo nyuma.
Kama unabisha muulize mkuu Nape Nnauye kilimpata Nini alipothubutu kutaka kuifatilia teknolojia aliyotumia ex koromijey militia.
 
Hahahahahahaha kuendelea kupata vichekesho kama hivyo bonyeza 15445
 
Nimekuja mbio nikidhani tumeshika nafasi ya Pili kwenye kutumia teknologia ya kijasusi kama ile aliyotumia mwana koromije mmoja kusepa na flash yenye kipindi chake bila kuacha nyayo nyuma.
Kama unabisha muulize mkuu @Nape @Nnauye kilimpata Nini alipothubutu kutaka kuifatilia teknolojia aliyotumia ex koromijey .
Hahahahahahaha mkuu
 
Haha labda wameangalia whatsup
Maana ata bibinga anayo kijijini
 
watanzania hatupendi nchi yetu yani kama tulizaliwa US alafu tukatupwa Tz, mtu hata akifnikiwa kutoka nje anajifnya anasahau na lugha kabisa!
 
watanzania hatupendi nchi yetu yani kama tulizaliwa US alafu tukatupwa Tz, mtu hata akifnikiwa kutoka nje anajifnya anasahau na lugha kabisa!
Mkuu hiyo avatar yako ukiwa "umevaa miwani" waweza toka nduki aisee kumbe ni memba mwenzetu wa hapa hapa JF.
 
Tanzania kuna mambo mengine tunafanya vizuri.....tujipongeze kwa balimi mbilimbili bili kwa Ngosha.
 
Back
Top Bottom