PostGE2025 Tanzania yapoteza zaidi ya TZS 560 bilioni kutokana na kuzimwa kwa mtandao wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Huu ni muhtasari wa athari za kiuchumi za kuzimwa kwa mtandao Tanzania siku na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 2025

▪︎ Nini Kilitokea?

•Tanzania ilikumbana na kuzimwa mtandao nchini kote wakati na baada ya siku ya uchaguzi mkuu kuanzia 29 Oktoba hadi 3 Novemba 2025, na intaneti ilizimwa kwa takribani siku 5-6
•Mtandao wa kijamii wa 𝕏 (zamani Twitter) umefungwa nchi nzima tangu 21 Mei 2025, huku kukiwa na upunguzwaji wa kasi ya mtandao (bandwidth throttling) kutoka kwa watoa huduma (ISPs)



▪︎ Hasara za kiuchumi

•Kwa mujibu wa Paradigm Initiative (PIN) na data kutoka NetBlocks Cost of Shutdown Tool (COST), hasara ya pamoja kutokana na kuzimwa kwa mtandao na kufungiwa kwa mtandao wa 𝕏 inazidi US$238 Milioni (takribani TZS 560 bilioni)

•Kuzimwa kwa mtandao pekee yake kunakadiriwa kugharimu takribani US$72 Milioni (takribani TZS 178 bilioni) kwa siku 5 za kuzimwa kwa mtandao - karibu US$13.8 Milioni kwa siku
•Kufungiwa kwa mtandao wa 𝕏 (the ongoing suspension of 𝕏) kulichangia hasara ya takribani US$165.8 Milioni (takribani TZS 390 bilioni) katika hasara za kiuchumi (economic losses)


▪︎ Nini kiliathirika?

•Kuzima mtandao kuliathiri sehemu kuu za uchumi wa kidijitali
•Uzalishaji na biashara katika majukwaa ya mitandaoni
•Huduma za malipo ya kifedha za kidijitali ambazo ni biashara kubwa na nyingi na watu binafsi hutegemea
•Huduma za afya na kijamii zinazotumia mifumo ya mtandao
•Minada ya kilimo na mauzo ya nje – biashara ya korosho, ilihairishwa kutokana na kukosekana kwa mtandao

▪︎ Maoni, hatua muhimu

•Makundi ya haki za kidijitali yanaeleza; kuzima mitandao kunakiuka uhuru wa kujieleza, kupata habar na haki ya maendeleo chini ya mifumo ya haki za binadamu ya kikanda
•Hatua za kisheria zimechukuliwa kupinga uhalali wa kuzima mitandao – mashauri yamefunguliwa Mahakama za ndani na nje

▪︎ Kwanini ni Muhimu?

Wachumi na watetezi wa haki wanaonya kwamba, vikwazo vya kujirudia katika matumizi ya huduma za kidijitali vinaweza;

•Kuzuia uwekezaji katika sekta ya teknolojia
•Kudhoofisha uaminifu katika masoko ya kidijitali
•kuzima ubunifu na ujasiriamali, miongoni mwa wafanyabiashara wadogo na watengeneza maudhui wanaotegemea majukwaa ya mitandao ya kijamii.
 
Amani, umoja na utulivu wa waTanzania vitalindwa kwa nguvu na gharama yoyote ile bila kujali hasara popote.

ni vizuri kuelewa jambo hili muhimu na la maana zaidi kuliko hasara au faida ya kitu kingine chochote
 
Amani, umoja na utulivu wa waTanzania vitalindwa kwa nguvu na gharama yoyote ile bila kujali hasara popote.

ni vizuri kuelewa jambo hili muhimu na la maana zaidi kuliko hasara au faida ya kitu kingine chochote
kama mwanadiplomasia sio nenda kaeleze ulimaliza watu zaidi 20000 kulinda Amani.
 
Kwa mujibu wa Paradigm Initiative (PIN) na data kutoka NetBlocks Cost of Shutdown Tool (COST), hasara ya pamoja kutokana na kuzimwa kwa mtandao na kufungiwa kwa mtandao wa 𝕏 inazidi US$238 Milioni (takribani TZS 560 bilioni)
Serikali huwa haina hasara...
 
kama mwanadiplomasia sio nenda kaeleze ulimaliza watu zaidi 20000 kulinda Amani.
kueliminate au kuneutralize bandits na terrorist hata laki1 tu ni jambo muhimu na la kupongezwa zaidi kwa usalama wa waTanzania na dunia nzima.
hakuna haja ya kunyenyekea mabeberu
 
kueliminate au kuneutralize bandits na terrorist hata laki1 tu ni jambo muhimu na la kupongezwa zaidi kwa usalama wa waTanzania na dunia nzima.
hakuna haja ya kunyenyekea mabeberu
Hujamuona Kombo anahaha kuko US. Anajikomba komba kwa wabunge na kutafuta vipicha vya hapa na pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…