khalfanially3
Member
- Mar 18, 2015
- 15
- 5
watanzania tunamatatizo mengi yanayotukabili, lakini tumeonekana zaidi tukiangalia Rais ameongea nini(sio watu wote) ili tumkosoe au tumpinge, nchi hii ikijengeka itajengwa na sisi wenyewe, Uchaguzi ulishaisha sasa ivi tujikite katika maendeleo jamani. sisi wote tulishiliki katika uchaguzi tukachagua na uchaguzi ukaisha. "Tanzania nakupenda tanzania, Napenda sana maendeleo na sio chama fulani, napenda sana watanzania pasipo kujali chama,dini wala kabila" huo ndio uwe wimbo wetu. Tumuache Rais atekeleze ahadi zake na tumuunge mkono kwakua maendeleo hayo ni yetu wote, kama hatokamilisha ahadi zake nadhani uchaguzi utapofika ndio tumchague huyo tutakaeona anatufaa,lakini kwasasa Yeye ndio kiongozi halali na ndio mkuu wetu. Mungu tubariki tanzania