Tanzania yangu na Afrika yangu naifananisha na mzee huyu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,743
25,535
Kuna mwanaume mmoja alikuwa masikini sana, kila siku asubuhi kazi yake ilikuwa ni kuombaomba mitaani. Alizoeleka katika mitaa mingi ya jiji kama alivyozoeleka Matonya kipidi kile.

Kila siku asubuhi, alikuwa akiamka na kuanza safari kuelekea mitaani, anapofika huko, uelekea katika eneo lake la kazi yake, huchukua kikombe chake na kazi ya kuomba fedha kwa watu wenye fedha kuanza.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku, aliendelea kuzoeleka sana na hata lilipokuwa likija suala la kuwaondoa ombaomba mitaani, mzee huyu hakuwa akiondolewa kwa kuwa alijulikana mno.

Siku zikakatika, kuna siku mzee huyu aliugua sana, hakwenda mtaani kuomba, maisha yake yakawa juu ya godoro lake chakavu lililotandikwa chini, tena katika nyumba chakavu iliyokuwa ikivuja maji kila mvua ilipokuwa ikinyesha.

Mtoto wake pekee ndiye aliyekuwa akimhudumia. Kila siku asubuhi alipokuwa akimsaidia baba yake kuombaomba mitaani na mchana anakuja na kumletea chakula kisha anaondoka tena na usiku anarejea kulala.

Baada ya siku kadhaa, mzee yule aliona kwamba asingeweza kuishi tena, alichokifanya ni kumuita kijana wake na kuanza kuongea naye.

“Ninakufa mtoto wangu, sina fedha za kukuachia, sina mali za kukuachia pia, ila kitu pekee ambacho ningependa kukuachia ni hiki kikombe changu cha kuombaomba. Niliachiwa na baba yangu ambaye naye aliachiwa na babu yangu, utakapokufa, naomba umuachie mtoto wako pia,” alisema yule mzee na hakuchukua dakika nyingi, akafariki dunia.

Kijana yule akawa ameirithi hiyo kazi, kama alivyokuwa akifanya baba yake, naye alikuwa akiamka asubuhi na kuelekea mitaani kuomba. Hayo ndiyo yalikuwa maisha pekee aliyokuwa ameachiwa na kuyazoea.

Hakudumu sana katika kazi ile, kijana yule naye akafariki dunia kwa ugonjwa wa saratani ya damu. Mara baada ya mazishi yake, watu wakaingia ndani ya chumba chake chakavu kuona aliacha kitu gani, hakukuwa na kitu cha thamani, kila kitu kilikuwa cha hovyo.

Kwenye kuangaliaangalia, wakakiona kikombe kile kilichokuwa kikitumika katika uombaji wa fedha mitaani. Kijana mmoja akakichukua kile kikombe, alipokibeba, hakikuwa kikombe cha kawaida, kilikuwa kizito mno.

Akaanza kukiangalia vizuri, akagundua kwamba kikombe kile kilikuwa kimewekwa vitu vigumu viivyozunguka kikombe kizima, akaanza kuvibandua vitu vile.

Akapigwa na mshangao, hakuonekana kuamini, kikombe kile kilikuwa ni cha almasi ila kilizungushiwa vitu vigumu. Almasi ile ilikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

Japokuwa mzee yule na mtoto wake walikuwa masikini, lakini hawakujua kama walikuwa na utajiri mkubwa waliokuwa wakitembea nao.

HII NI SAWA NA TANZANIA AU AFRIKA KWA UJUMLA. TUNA KILA KITU KUANZIA DHAHABU, ALMASI, GESI NA VITU VINGI SANA LAKINI SISI WENYEWE BADO NI MASIKINI WA KUTUPWA HUKU KILA SIKU TUKIOMBA MISAADA.
INASIKITISHA MNO!


The Monk Who Sold His Ferrari
 
Ka story kazuri kamenisaidia kupunguza stress maana no usingizi. Anyway, tuendelee kupambana huenda IPO siku tukaitumia vema rasimali yetu

Hapa Natamani kama pakuche niende zangu kufanya kazi,naona kitanda kinazingua tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom