Tanzania yakosa tena Rais 2005 - 2015

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Baada ya hayati Mwalimu Nyerere Tanzania ilikosa Rais kwa muda wa miaka 10 mpaka 1995 ambapo tulipata Rais, Ben Mkapa. Phase II ilijaa uenyeji na kusigina katiba. Sasa Phase IV ina-reflcet Phase II kwani ni kama hakuna Rais.

Hivi Rais na mamlaka yote makubwa aliyopewa na katiba mpaka wananchi wanataka kuyapunguza anawezeje kulalamika kwa wananchi? Wananchi wawafanyeje watendaji aliowaweka yeye mwenyewe na ana mamlaka ya kuwaondoa? Je, katiba si ina mruhusu kufanya re-shuffle ya cabinet of ministers muda wowote na bila kuulizwa? Hivi Rais huyu Jakaya Mrisho Kikwete anaifahamu kweli katiba hii? Je, anachokifanya sio kuvunja katiba ya nchi hii?

Kutengeneza ombwe la uongozi (power vacuum) ni sawa na kukuzalilisha kiti cha Urais na katiba inasema kuwa kiti cha Rais kitakuwa wazi na uchaguzi kufanyika tena endapo Rais hawezi kumudu kazi zake ibara ya 38 (2) (e) na 37. Pia Rais ataachia ngazi au kuachishwa ngazi kwa mujibu wa masharti ya katiba 42 (3) (d).

Halafu JK asivyokuwa makini na maendeleo ya mawasialiano anawataka mawaziri wachome mafuta na ma-V8 kuzunguka nchi nzima kusikiliza kero za wananchi kama vile vyombo vya habari havipo Tanzania. Kuna TV, Radio, Internet, world wide web - social media kama JF, mobile phone; hivi badala ya kuzunguka kwa nini wasitumie njia hizi au ndio kuwaiga Chadema? Hivi kazi ya ili li website walioanzisha na kujibandika picha yake kwenye home page ni la nini? je wananchi wanalitumia? je walioko vijijini wanaweza kuli-access na kulitumia? Lili-link lenyewew ili hapa KILA MWANANCHI AWEZE KUTUMA MAONI YAKE... Je, linatumika na hata hao wenye internet access? je, liko effective na efficient?

Kuna msemo unasema kuwa "birds of the same feathers flock together". Huu unatoa uharisia kwenye Phase IV ya Tanzania leadership. Kama aliowachagua ni wazinzi, walevi, wezi, wababe, dhulumati, yeye hakuliona hili? Je, katiba inamtaka afanye nini? Hivi wakati ule wa uchaguzi mkuu 2010 yeye kama mwenyekti wa CCM si aliongoza kumtupia tuhuma Dr. W. Slaa kuwa ni mzinzi - kapora mke wa mtu, hivi hakujua kuwa wazinzi waliobobea wako ndani ya CCM?

Wabunge tumieni katiba kumwondoa JK madarakani kwani mamalaka hayo kikatiba mnayo. Mawaziri pia wanamamlaka hayo kikatiba lakini hawawezi kufanya hivyo kwani wanafahamu JK hamna kitu; kwani akija mwingine wote watasahau madaraka hayo mpaka kuingia kaburini.
 
Back
Top Bottom