wananchi wanateseka kwa umasikini, uchumi umekufa na kuna mfumuko mkubwa wa bei.
Shangaa kipato cha wananchi wengi kimeshuka na bidhaa muhimu zimepanda bei
uzalishaji umeshuka kwa sababu mafuta yamepanda bei na umeme ni mgao, ni kama hakuna.
Hakuna umeme mbadala kama solar power au gas
viongozi wanafanya ufisadi mchana kweupe, hawaogopi tena
viongozi wanaiba na kulindana, ina maana wanatimiza ile dhana chukua chako mapema
mashirika na viwanda vimekufa, ajira hakuna.
Vijana wanahangaika, nguvu kazi inapotea
wazee ndo hao wanaingia mikataba mibovu kwa sababu ni wavivu kusoma na wanatumia masaburi kufikiri
wazee wanang'ang'ania madaraka hawataki kupumzika wakalee wajukuu
wazee wamekula mpaka wamevimbiwa, wanakufuru mpaka wanalea vimada, tena wanaharibu wasichana wadogo wenye umri wa binti zao
mabinti hawana jinsi, wanakubali kutumika kwa sababu wana njaa, umasikini umewakabili.
Nikiendelea kusema nitalia, wacha niachie hapa.
Labda wasomaji na wachangiaji wengine wanaweza kuongezea.
Source: Tanzania daima na mwananchi paper leo