Tanzania ya viwanda yenye mgao wa umeme

GedsellianTz

JF-Expert Member
Jul 5, 2016
1,348
1,803
Namsoma Michael Hyatt na maswali yake magumu yanayohitaji utashi mkubwa kuyajibu.
1. How do you encourage creative thinking within your Country?
2. What is one characteristic that you believe every leader should possess?
3.What is the biggest challenge facing leaders today?
4.What is one mistake you witness leaders making more frequently than others?

Tanzania Mungu ametupa kila kitu cha kutufanya tuwe wanadamu matajiri kuliko wote duniani ila tumekosa kuwa na viongozi wabunifu na wenye tija katika kuongoza wa Tanzania wanaonuka umaskini na wenye shida ya matatizo ya kila namna,siku zinavyozidi kwenda ndivyo wa Tanzania wanavyozidi kufubaa kwa matatizo na umakini usio kwisha.

Waziri mzigo wa awamu iliyopita anawezaje kuwa na tija awamu inayokuja ? badala ya kuchagua watu wapya na wenye utashi mkubwa na ubunifu wa hali ya juu ila tunahamisha tatizo la awamu ya 3 na kupeleka awamu ya 4 kuna baadhi ya mawaziri hawakutakiwa kurejea kwenye uwaziri ,ili kupisha mawazo mapya na changamoto mpya na kuwa na suruhisho la matatizo ya zamani.

Hatuwezi kuendelea hata siku moja kuwa na viongozi wenye tija sababu ya viongozi wengi wanajirudia rudia na hawana tija ya kutatua matatizo yetu bali wana uzoefu wa kuongeza matatizo yetu .Kuna watanzania wengi wenye upeo mkubwa wa kutatua matatizo yetu na wana wigo mpana sana wa maarifa ila hawapewi nafasi ya kuongoza kwa sababu zilizowazi .

Najiuliza ni nani mtu jasiri anayeweza kuwaita maraisi wote walio wahi kutuongoza na kuwauliza maswali walishindwa wapi kutupa maisha mazuri na yenye tija na kutengeneza kizazi bora kwa nyanja zote walizo kuwa madarakani?TBC ilitakiwa iwe inaandaa midahalo yenye tija kwa viongozi waliopo madarakani na waliowahi kuwa madarakani ili kuweza kujua matatizo yetu.

Kujua tatizo ni jambo moja na kulitatua ni jambo jingine .Nabii Samweli alipokuwa anakaribia mwisho wa kipindi chake cha uongozi wake aliwauliza watu aliokuwa anawaongoza akiwa katika mkutano wa hadhara aliwauliza hivi "Ni nani niliyemdhulumu ?Ni nani niliyemwonea? au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho?Nami nitawarudishia ninyi [ 1 samweli 12:3]

I am the one writing my story. Sadly I’m writing in pen and can’t erase my mistakes.
 
Back
Top Bottom