Tanzania ya viwanda: Wananchi wa Momba waanzisha kiwanda kwa nguvu zao wenyewe


K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Messages
1,691
Likes
2,207
Points
280
K

kirerenya

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2013
1,691 2,207 280
chumvi-jpg.631308

WANANCHI wa kijiji cha Ivuna Wilayani Momba Mkoani Songwe, wamefufua kiwanda cha uzalishaji wa chumvi katika eneo la Bwawa la Maji chumvi kilichokuwa kimesitisha shughuli zake za uzalishaji kutokana na uhaba wa fedha.

Wakiongea na Mwandishi wa habari hii, wananchi hao walieleza kuwa mradi huo wa uzalishaji chumvi ulikuwepo tangu awali na kwamba uzalishaji wa chumvi katika eneo hilo ulisitishwa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.

Walisema wameamua wameamua kutumia kutumia nguvu zao wenyewe badala ya kuitregemea serikali kufufua upya mradi huo kwani wanaamini kuwa utawasaidia kuondokana na umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wanaoishi katika kijiji hicho.

Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hicho Hussein masayanyika ambaye pia ni mkazi wa eneo hilo alisema wanamatarajio makubwa ya kunufaika na mradi huo wa uchimbaji wa chumvi kwani biashara ya chumvi ni biashara ambayo haisumbui sana kutafuta masoko kwa vile chumvi ni kiungo kinachohitajika kila siku katika matumizi ya chakula.

“Sisi tumeamua kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kufufua kiwanda hiki tunaomba sasa Serikali itusapoti itupatie vitendea kazi hasa mashine za kuchimbia chumvi changamoto tuliyonayo hapa ni vitendea kazi hivi sasa tunachimba kwa kutumia majembe na sululu hali inayofanya tuone kazi hii kuwa ni ngumu”Alisema Masayanyika.

Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Ivuna Julius Baltazari alisema Uanzishwaji wa kiwanda hicho ni moja ya utekelezaji wa sera ya serikali ya awamu ya tano ambayo kaulimbiu yake ni Tanzania ya viwanda ambapo viongozi ndani ya Mkoa wa Songwe wamelibeba hilo kama agenda katika kila kusanyiko wakisisitiza wananchi kuanzisha viwanda vidogovidogo kuinua uchumi wa wananchi kutoka ulipo kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2020.

Aidha aliwataka wawekezaji wote wenye uwezo wa kuwekeza katika eneo hilo kuja kuwekeza kwa vile wanahitaji zaidi wawekezaji hususani wawekezaji wazawa ili kuendeleza kiwanda hicho na kuongeza kuwa awali chumvi hiyo ilikwisha fanyiwa utafiti na wataalamu ambapo ilionekana kuwa eneo hilo linauwezo wa kuzalisha chumvi yenye kiwango cha ubora wa daraja la tatu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mombo Adrian Jungu alisema kuwa viongozi ndani ya mkoa wa songwewapo tayari kushirikiana na wananchi hao na kuwapa sapoti kwani wanatekeleza agenda ya uanzishwaji wa viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo katika kuinua uchumi wa wananchi kutoka ulipo kuelekea uchumi wa kati .

Alisema katika bajeti ya fedha ya mwaka 2017/2018 halmashauri imetenga kiasi cha shilingi million 50 kwa ajili ya kusaidia kununua mashine ya itakayosaidia katika shughuli za uzalishaji wa chumvi katika eneo hilo.
 
Maxmizer

Maxmizer

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
3,979
Likes
3,286
Points
280
Maxmizer

Maxmizer

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
3,979 3,286 280
safi sana serikali toeni sapoti kwa vijana wenzetu hawa
 
double R

double R

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Messages
1,673
Likes
1,112
Points
280
double R

double R

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2011
1,673 1,112 280
Kwa huko Momba kulivyo, hongera zao
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,779
Likes
25,180
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,779 25,180 280
CCM ni balaa haswa.
 
U

uhurubado

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2007
Messages
479
Likes
264
Points
80
U

uhurubado

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2007
479 264 80
Kudos vijana. Mapinduzi ya viwanda yataletwa na wenye moyo!
 
omarion5

omarion5

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2017
Messages
5,051
Likes
17,344
Points
280
omarion5

omarion5

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2017
5,051 17,344 280
Serikali Viwanda ndo hii ya sehemu ya tano?
 

Forum statistics

Threads 1,236,915
Members 475,327
Posts 29,272,536