Tanzania ya Viwanda Haijengwi kwa Propaganda

Tanzania ya Viwanda Haijengwi kwa Propaganda

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,381
Reaction score
4,664
Habari za usiku huu:

Hivi kuna ukweli kwamba kama mtu hajalala usiku basi ni Popo na kama ni Bundi ni Mchawi?

Hivi kuna ukweli kwamba viongozi wetu wanahubiri Tanzania ya Viwanda kwenye Majukwaa lakini kwenye utekelezaji wanahubiri Tanzania ya Ujima.Haya kabla sijashtakiwa kwa uchokonozi basi nitoe ushauri ufuatao

Tunapozungumzia ujenzi wa uchumi wa viwanda lazima tujiulize misingi ya uchumi wa viwanda ni ipi na inachukua muda gani kwa taifa kujiita taifa la viwanda.

Ili kufikia hatua ya kuwa nchi ya kiwanda lazima tupitie kwanza ujenzo wa nyenzo za uzalishaji.Nyenzo za kwanza za kuboresha ni nyenzo za uzalishaji wa kilimo.Kwa hiyo kwa kuanza lazima tuwekeze katika uzalishaji wa kilimo ili tuwe na chakula na mali ghafi za kutosha.Hivyo basi serikali lazima inaposema kilimo kwanza ianze na wakulimu kwa kuwapatia mashine za kilimo,Tunaweza kuanza na Trekta moja kwa kila kijiji au basi kwa kila Kata.Na nafikiri kwa Mh,Magufuli anaweza kutekeleza hili kama mbadala wa ile ahadi ya milioni hamsini kwa kila kijiji.Kwa hiyo ushauri wa kwanza kwa bwana JPM peleka zile milion 50 kama trekta kwa kila kijiji hapa Tanzania.Wenye Takwimu mmwambia kuna vijiji vingapi Tanzania.Hilo linawezekana.

Jambo la pili ni kuwekeza kwenye elimu.Ni upumbavu kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu kutoa mikopo kwa watu wa degree tu halafu kisha zaidi ya 75% wanaingia mitini hawataki kulipa ni matumizi mambaya ya rasilimali.Ni hii inakuwa mbaya zaidi pale ambapo mafunzi ya ufundi stadi yako underfunded.Je si ni bora kusomesha mafundi mchundo veta na kisha wakishajiajiri waombe mkopo kujiendeleza kwa ngazi zajuu za elimu kuliko kuwa na wasomi njaa milioni ambao hawana ajira wala uwazi wa kuzlisha ajira.Kwa hiyo bwana JPM la pili la kufanya FUTILIA MBALI HESLB na kisha anzisha EDUCATION AND TRAININF FUNDING AUTHORITY ambayo badala ya kutoa mkopo kwa watu wa elimu ya JUU itoe mkopo kwa watu hata wanaosoma Vocationa Colleges ambao watafundishwa mafunzo productive.Hawa mnaowalipia mabiliano halafu wanakosa ajira wanaishia kutumia elimu yao kuwatukana huku kwenye mitandao

Jambo la Tatu ni mfumo wakodi.Nafikiri tanzania ni moja kati ya nchi ngumu sana kuanzisha biashara rasmi.Urasimu na gharama za kuanzisha biashara ni kubwa sana.Najiuliza ni kwa nini kuwa na ugumu na gharama za kuanzisha biashara kama mnataka kujenga nchi ya viwanda.Nishauri kwanza Business Licence kama ilivyo tin number na VAT,zitolewe bure kwa wajasiriamali kwa sababu sioni sababu ya kulipia leseni ya biashara.Kitu cha muhimu hakikisheni watu wanaambatanisha bank statements zenye kuonyesha kuwa wana kipato cha kufanya biashara na maafisa wenu watembelee locatio kukagua kama zina vigezo kwa leseni inayoombwa baada ya kufanyiwa ukaguzi wote basi Mjasiriamali atozwe inspection fee na apewe inspectioncertificate kuonyesha kwamba mmekagua sehemu ya biashara na kwamba inafaa kwa biashara na kwamba mtu ana mtaji wa kufanya biashara na ana uwezo na nia ya kufanya biashara.Kwenye kodi mtu anaweza pea Tax relief kulingana na stage yake ya biashara kama ni biashara mpya mpeni hata mwaka au miaka miwili ya kutokulipa kodi bila kusumbuliwa lakini alete taarifa ya mapato matumizi nafaida au hasara wakati wa kuomba leseni ya kuendeleza kwa mwaka wa pili.

Jambo lingine anzeni kuhamasiha watu kuchangia kwa hiyari kwa kuwapatia taxi credit wale watu wanaochangia maendelea ya jamii naamini hili linawezekana ili kufundisha watu kulipa kodi na kuchangia maendeeleo

Swala la tatu ni kuhakikisha kuwa kila mkoa unatumia rasilimali zake kuzalisha mali kama mkoa sio mzuri kwa kilimo basi upewe kipaumbele ya viwanda ili kutengeneza ajira katika eneo hilo

Mwisho lakini si kwa umuhimu ni URASIMI URASIMI URASIMU.Hata Mzee JPM pamoja na biti zake bado hajaweza kuupiga vita Urasimu na huu ndio adui namba moja ya maendeleo yetu

Wasalaam

PBK
 
Itajengwa kwa kununua wapinzani[emoji2][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Trump anakubalika 39%
Huyo fulani itakuwa 9%
 
Back
Top Bottom