Tanzania ya Uchumi wa Viwanda: Ndoto itakayotoweka kabla hakujachwa!

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Tumekuwa na tatizo na huenda tukakwama huko tunapoelekea.
Serikali yetu imekuwa na dhamira njema sana na kutaka kuona tunapiga hatua kubwa ktk just mwaka 1 tu wa serikali mpya, lkn so far naona tunahitaji kurudi mezani kuchora upya ramani ya ushindi!

Mikakati yetu ya viwanda na mikakati mingine ya kukuza uchumi pamoja na nia njema tuliyonayo yapaswa kutazamwa upya na focus kuu juu ya ufufuaji huu wa uchumi!

Kwanza hatuwezi kufanya kila kitu ktk term 1 au hata hizo term 2 kama JPM atapita 2020. Tunapaswa kurejea tena na kutafakari ni uchumi gani tunaotaka kuujenga?

Uchumi wa Viwanda vya aina gani?
Ni mali ghafi zipi zinahitajika katika Viwanda vyetu hivii na upatikanaji wake ukoje?

Nani ana invest ktk Viwanda hivi?

Je haitoshi kujenga tu mazingira bora kwa investors waje kujenga Viwanda? Ni lazima vimilikiwe na umma? Ili tupate tija ipi? Heshima ya umiliki au kukuza uchumi?

Hebu wachumi tusaidieni katika kumshauri raisi na viongozi wengine wa awamu hii, wana nia njema lkn skills bado zinatutupa mkono!
 
Kitu cha kwanza na cha muhimu ni kiongozi wa juu kuwa na "willingness" (utayari) wa kufanya mabadiliko..kusafisha uchafu, kuondoa uzembe, kujenga nidhamu na accountability (uwajibikaji)...tukishakuwa na intact structure, safi na inayojitegemea (kwa kiasi kikubwa) suala la "ability" (uwezo) linafuata baadae -automatically..
So far (hata wewe unakubali) kuwa kiongozi wa juu ameonyesha nia na utayari wa kufanya mabadiliko...mimi na wewe ndo tutaleta utofauti kama tuko tayari kubadilika au tutaendelea ku subotage (kuhujumu) hii mikakati..hiki sio kitu cha siku moja, kama ulidhali viwanda vinajengwa kwa miezi 6 basi umepotea..
 
Mzee umeshakuwa negative na mawazo yangu!
Mi nadhani ifike saa tujue kuwa hakuna mwenye haki zaidi au anayeipenda nchi zaidi ya mwingine!
Ukisoma mjadala wangu nimeomba watu wenye taaluma za uchumi wasaidie katika kufikia malengo muafaka
Hata kama watu wakiwa na nidhamu kiasi kipi, kama hatuna resources hatuwezi kufanikiwa! Lkn pia tunaweza kujenga Viwanda lkn tusizalishe kwa tija! Lkn Viwanda sio lazima viwe vya watanzania, vikiwa Tanzania tu inatosha!
Wachumi kwanza waanze na maoni yao, sio sisi wanasiasa wa kudandia kupiga domo!
Mimi nimekiri hapo kuwa sio miezi 6, hata term 2 za uongozi hazitoweza kuleta mapinduzi ya Viwanda, bali tunaweza kujenga misingi imara ya ufufuaji uchumi kupitia sekta hiyo!
 
Change your mind set. Au ukae kupiga domo kijiweni.
Nafikiria nimechoshwa na hili la kuwa 'Hatuwezi' hatuwezi hatuwezi kila kukicha. Hivyo basi, kaa usubiri 2020 halafu useme kama kukicha na viwanda havipo wakati huo. Nitakuomba radhi.
 
Back
Top Bottom