Tanzania ya mwisho kwa kutuma barua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania ya mwisho kwa kutuma barua

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Oct 10, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tanzania ya mwisho kwa kutuma barua Friday, 09 October 2009 16:19 Benjamin Masese na Khadija Kikwekwe

  TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya mwisho duniani kutumia huduma ya posta ya kusafirisha barua, nyaraka na vipeperushi na kusababisha kudumaa kwa shirika hilo.

  Takwimu zilizopo sasa zinzonyesha kuwa wastani wa barua kwa kila Mtanzania kwa mwaka anatuma barua moja huku nchi zinazoongoza kwa viwanda ikiwemo Ulaya na Marekani wakituma barua 403 kwa mwaka kwa mtu mmoja.

  Vile vile hali hiyo imejionesha katika nchi nyingine zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ambako kuna asilimia10 ya idadi ya watu wote duniani ambapo Bara la Afrika lina asilimia moja ya idadi ya barua za ndani ambazo kila mtu huandika au kupokea wastani wa barua tatu.

  Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt.Patrick Makungu.

  Dkt.Makungu alisema kuwa mawasiliano kwa njia ya Posta ni nyenzo muhimu na rahisi sana ambayo inaweza kutumiwa na jamii yoyote katika kufanikisha masuala ya kijamii na kiuchumi.

  "Hakuna njia mbadala au ya mkato kurekebisha huduma za posta,bali inabidi zichukuliwe hatua za awali kuwajengea wananchi na hasa vijana wa shule tabia ya kuandika barua zenye mada na maudhui mbalimbali,"alisema.

  Pia alisema kuwa takwimu zilizoandaliwa na Umoja wa Posta Duniani(Universal Postal Union) zinaonyesha kuwa kiwango cha barua katika nchi zilizoendelea kinatofautiana na kiwango cha nchi zilizo maskini.

  Katika hatua nyingine wanafunzi wa shule mbalimbali wamezadiwa zawadi zikiwemo fedha taslimu,vyeti,na vifaa vingine baada ya kushiriki katika uandishi wa barua duniani na kuwa washindi kati ya kumi bora.

  Wanafunzi hao ni Rukaiyah Khoja wa shule ya msingi Popatlal ya Mkoani Tanga,Doreen Malavanu wa shule ya msingi Brooke Bond ya Mkoani Iringa na Mahfudh Nassor wa shule ya Brooke Bond.

  Hata hivyo ameiomba Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi kuandaa mashindano shuleni ya uandishi wa barua kitaifa sambamba na kuwashirikisha watalaamu wa posta kutoa semina pamoja na Tawala za mikoa na serikali za mitaa.

  Alisema kuwa huduma za posta zinaweza kupunguza kero katika jamii hasa ikizingatiwa kuwa mitandao ya posta hapa nchini ina ofisi 250 ambazo ni sehemu ya ofisi za posta 660,000 duniani.

  "Lengo letu kuu liwe ni kupanua vipaji na ubunifu wa vijana wetu ili waweze kushiriki ipasavyo kwenye utandawazi katika dunia ya soko huria na yenye mapinduzi ya kiteknolojia pia vijana sharti wawe wadau wa maendeleo sio kuwa watazamaji tu,"alisema.

  Tangu shirika la posta kuanzishwa duniani Octoba 9 1874 limefikia umri wa miaka 135 ambapo Tanzania ilijiunga mwaka 1963,kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa inasema 'Huduma za posta zinazingatia utunzaji wa mazingira'.

  Source:Majira

  Maoni na maswali yangu: Hii inasababishwa na ufisadi wa viongozi,wizi wa parcel za ndani kwa ndani na sana sana za kutoka nje ya nchi unaofanywa na wafanyakazi,wizi wa barua zinazoonekana zina uzito kidogo wakidhani kuwa kuna vitu vya dhamani. Je kipi kifanyike kukomesha haya? Je yaliyosemwa na Naibu Katibu mkuu ndio suluhisho? Hapo pekundu ndio njia yenyewe ya kurekebisha au kuna kitu anachokikwepa?
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Labda tushaingia katika singularity ya post literate society, ambako kila kitu kinaenda kwa email na Facebook, lol. Au kwa teknolojia ya ungo.

  On a serious note though, I see a trend where the very poor and the very rich will end up with the same statistics for different reasons.

  Wenzetu wataacha kutuma barua kwa sababu watakuwa wanatumia email, sisi tutaacha kutuma barua kwa sababu hatuna hela za stamp, barabara za kusafirishia barua na hatujui kusoma/ kuandika.

  Wenzetu wataacha kusoma na kuandika kwa kuwa watategemea zaidi audio/video means.Siisi tutaacha kusoma na kuandika kwa sababu ya poor planning and allocation of our meagre resources.

  At the end of the day the whole polarity North/ South thing is going to merge into one big idiocracy.Perhaps the asians can save us.
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Barua unatuma leo kutoka Dar kwenda Mwanza inafika baada ya wiki nne(mwezi mzima)
   
Loading...