Tanzania ya miaka ya 1980

Wimbi la vijana kwenda ng'ambo lilishamiri katika kipindi hiki.
 
Mabere Malando[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] na shahidi X pia alitoa ushahidi
 
Wimbi la vijana kwenda ng'ambo lilishamiri katika kipindi hiki.
'Stole away'.
Nna jamaa zangu wawili walikwenda kudandia meli Maputo, mmoja alidakwa mpakani (Mtwara) akarudishwa na mwingine alienda mpaka Italy lakini na yeye wakamrudisha.
 
Mungu atuweke hai na sisi tutakuja kusimulia enzi hii kwa kwa wajukuu maana huyu Makufuli sio wa kusahau
 
Miaka ya 80 mazao yalikuwa yanaota kwa lengo la kulisha watu, lakini baada ya laana ya watawala sasa mazao yanaota kwa ajiri ya mbegu ili ihifadhi kizazi chake.
 
80s pamoja na kuwa tulitoka Vitani Tukakaza Mikanda,maduka ya Kaya,Uhujumu uchumi nk.
Tanzania ndio tulikuwa tumefika mahali pazuri Kiviwanda kwani Mashirika mengi ya Umma yalikuwa yako imara na viwanda alivyojenga Mwl ndio vilikuwa kwenye pick!

Miaka hiyo watumishi waliofanya kazi kwenye Mashirika ya Umma(SU) na vyama vya Ushirika ndio waliokuwa wanaheshimika kwa kuwa na kupato kikubwa wafatie watumishi wa Chama na Serikali..

Ajira kama Ualimu,Police,Jeshi,Mahakama zilidharauliwa sana na ndilo lililopelekea mwanzoni mwa 90s, baadhi ya idara kama Police,Mahakama na Magereza, na Mamlaka ya Kodi(TRA) kuwa na baadhi ya watumishi walioingia kwenye rushwa wakirubuniwa na hao wengine na wafanyabiashara hasa wale wa Kiasia na waarabu walioshika biashara wakati ule.

Mwl. Alipigia kelele sana hali akisisitiza kuwa "Rushwa ni hatari sana kwani ikishaingia ni vugumu kutoka"

Miaka ya 90s baada ya rushwa kuingia na kuwa na watumishi wa Mashirika ya Umma walioshirikiana na wafanyabiashara na baadhi ya Viongozi wasio waaminifu, ndipo ilipotokea muanguko wa Mashirika mengi sana na baadaye tulipolazimishwa kuingia kwenye privatization ndip ikapelekea kuua viwanda vyetu vingi.

Anachokifanya Raisi wetu Magufuli, wengi wanakielewa ama wanakataa kukubali kukielewa.
Huyu anavunja na kuondoa biashara zinazotoka nje ambazo malighafi zake au rasilimali zake tunazo, na kualika wawejezaji wa ndani na nje kuwekeza katika kuganya production ya bidhaa hizo hapa nchini ili hatimaye na sisi tuzipate hapanhapa kwa bei nafuu na pia Wafanya biashara wa ndani na nje wazichukue na kufanya exports.

Haya hayaji miraculous kwamba leo kesho tayari, ni lazima kuharibike kitu, halafu kujengwe kitu ndio mavuno yaje. Hivyo tuchangamkie na kutafuta mapya ya fursa zijazo na tusipayuke tukiacha wajanja wanakamata hizo fursa zilizopo na zijazo huku wakiturubuni na kutupotosha tubaki watumwa wao baadaye.


Mradi wa trilioni 3 wasajiliwa nchini, kutoa ajira 4500
Vitu kama hivi alichoppst Trump2 ndivyo tungekuwa tunachangamkia kutafuta kujua mbali ya ajira vina fursa gani zingine , na kisha mchanhamkie au muwapeleke ndugu wasio na ajira au wenye mitaji wafanye biashara nk. badala ya kukaa na kuponda .

Angalieni wenzetu wa Jukwaa la Kenya humu JF , mbali ya Politics zaidi wanalitumia kuhabarishana fursa za biashara na uchumi na nyingi zikiwa ni za hapa kwetu. Sisi habari hiyo hiyo tutangoja kina Zito waseme na wasiposema inakuwa sio habari, kibaya ikiletwa kwenye mjadala itapondwa na kupuuziwa huku wapuuzaji wengi ni wale hohehahe wasio na lolote.
Vijana amkeni
 
Bila ya kusahau jamaa wa mali ya sili Walikuwa wanakuja na migobole mijini hasa Dodoma na kuwapiga risasi mbwa wazuzuraji.
 
Dah....umenikumbusha mbali sana...chozi limenidondoka[emoji87]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…