Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mtu akiwa angani ndani ya ndege wakati anawasili kwenye majiji makubwa kama New York na Moscow huanza kuyashuhudia magorofa makubwa, wakati ndege inaanza kuusogelea uwanja kabla ya kutua. Wenyewe huviita vikwangua anga (sky scrapers).
Majengo hayo pamoja na madaraja mazuri yanayopendezesha majiji makubwa duniani, yalijengwa miaka mingi iliyopita, tena kuna hadithi za ukweli kuhusiana na watumwa kumwaga jasho lao wakati wa ujenzi. Majengo, madaraja na miundo mbinu yote hiyo ilijengwa miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo miaka mingi tangu walioyajenga wafariki dunia, bado kazi iliyofanyika inaheshimiwa kwani inatumiwa na wajukuu zao ambao nao pia wanao uhakika kuwa wajukuu zao watakuja kuufurahia uzuri wa kazi iliyofanyika miaka mingi iliyopita.
Leo hii yanajengwa madaraja na majengo mazuri kila mkoa wa Tanzania. Gharama inayotumiwa ni kubwa sana, lakini kilichoangaliwa ni ubora wa majiji yetu ndani ya miaka 50 au zaidi ijayo. Wapo wanaolaumu kuwa majengo makubwa hayana wapangaji, wapo wanaosema kuwa ujenzi wa madaraja makubwa ni upotezaji wa fedha za walipa kodi. Je madaraja, majengo na miundo mbinu mizuri isipojengwa leo, upo uwezekano wa Tanzania ijayo kuwa na miundo mbinu bora kwa watakaokuwepo nyakati hizo.
Sidhani kama ni sahihi kuishi na mawazo ya kibinafsi kwamba majengo, madaraja na miundo mbinu inayojengwa sasa kwa gharama kubwa ni lazima eti irudishe faida ndani ya uhai wa watu wa kizazi cha sasa. Waliotumia nguvu na kuingia gharama ya kujenga majiji makubwa duniani walijua kuwa watakaofaidi ni wale watakaokuja kuishi miaka zaidi ya 100 baadae.
Kwanini tunaiangalia Tanzania kibinafsi?. Kwanini tusijenge fikra vichwani mwetu kwamba nguvu inayotumika katika kubadilisha majiji na miji yetu ili iwe ya kisasa, ni nguvu inayoitazama Tanzania ya miaka 100 na zaidi ijayo?. Ni mawazo tu waungwana.