Tanzania ya Magufuli safi, lakini...

Tanzania ya Magufuli safi, lakini...

chikub

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
110
Reaction score
28
Magufuli amezikonga nyoyo zetu lakini atazingonga zaidi kama atatengeneza katiba ambayo kila jambo zuri kwa nchi linazaliwa ndani ya katiba na kila jambo baya kwa nchi linazuiliwa ndani ya katiba. Hatutegemei kwa miaka 5 ya Magufuli ataweza kurekebisha nchi iliyoharibiwa na chama chake kwa miaka 10 ya Mwinyi, 10 ya Mkapa na 10 ya JK, ila anaweza kuchagua vitu vichache tu vya kufanikisha kama vile katiba, ufisadi, afya na elimu tu, na watu watamuelewa tu.
 
Nasikitika sana maana ni kama anapigana mwenyewe kwenye hii movie. Sina ahaikia ni wanacm wangapi wanamuunga mkono toka rohoni. Bunge likianza makapi mengi sana yatakua juu, lets wait and see what will real happen.
 
pumba. nani kakuambia akina mwinyi, mkapa na kikwete wameharibu nchi? mngeyaona ya kule burundi, sudani kusini au somalia mngeelewa somo. maana akili zenu za hovyo kweli. hao kila mmoja ametekeleza majukumu yake na magufuli naye ananafasi yakufanya yake atuachie nchi yetu ikiwa salama.

Magufuli amezikonga nyoyo zetu lakini atazingonga zaidi kama atatengeneza katiba ambayo kila jambo zuri kwa nchi linazaliwa ndani ya katiba na kila jambo baya kwa nchi linazuiliwa ndani ya katiba. Hatutegemei kwa miaka 5 ya Magufuli ataweza kurekebisha nchi iliyoharibiwa na chama chake kwa miaka 10 ya Mwinyi, 10 ya Mkapa na 10 ya JK, ila anaweza kuchagua vitu vichache tu vya kufanikisha kama vile katiba, ufisadi, afya na elimu tu, na watu watamuelewa tu.
 
WAZIRI WA SHERIA Mh. MWAKYEMBE BAADA YA KUAPISHWA, ALIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI, "katiba itaanza pale ilipo ishia imeishia mahala pazuri, tutaimalizia muda utakapofika"WAZIRI AMESHAAHIDI WE UNATEGEMEA NINI KAMA ITAANZIA PALE ILIPOISHIA?
 
pumba. nani kakuambia akina mwinyi, mkapa na kikwete wameharibu nchi? mngeyaona ya kule burundi, sudani kusini au somalia mngeelewa somo. maana akili zenu za hovyo kweli. hao kila mmoja ametekeleza majukumu yake na magufuli naye ananafasi yakufanya yake atuachie nchi yetu ikiwa salama.

Burundi kua katika hali mbaya kuliko sisi haimaanishi tupo katika hali nzuri.
Ni kama moja kapata C mwingine F huku passing grade ni B, japo C yupo vizuri kuliko F ila bado hajapass vilevile tu. Watanzania wengi maskini wa kutupa, asilimia kubwa wanaamka hawajui hata kama watafanikisha mlo moja kwa siku, nchi ambazo tunaweza sema ni successful japo wana maskini ndio lakini bado maskini wengi hawasumbuki kwenye swala la msosi.

Tanzania na vyanzo vyote vya fresh water, sehemu ambazo hawana maji salama ya kunywa ni nyingi mno, kuna nchi nyingi tu wanahamu wangekua na vyanzo kama vyetu maana unakuta wana vyanzo kama asilimia 20 ya tulivyonavyo lakini wamefanikiwa ku-supply nchi nzima na maji hayakatiki 24/7. Mwanza tu pamoja na kua na Ziwa Victoria maji yanakatika karibia kila wiki, ni aibu kubwa mno. Bado tunacheza sana

Marais waliopita sisemi wamevuruga sana, wamejitahidi kadri ya uwezo na nawapongeza kwa hilo najua kuongoza nchi sio swala rahisi lakini bado walichokifanya hakitoshi kabisa.
 
mstari wako wa mwisho umeeleza kila kitu. sio kuponda tu kila kitu. pamoja na kuwa tunailaumu serikali lakini hata sisi wananchi pia sehemu yetu kubwa hatutimizi majukumu yenu. sasa mtu kama wa pwani ambapo maji ni ya uhakika anashindwa hata kujishughulisha kulima mboga mboga na hapo akila mlo mmoja anailaumu serikali. kama sio upuuzi ni nini? mengine tumejitakia wenyewe.

Burundi kua katika hali mbaya kuliko sisi haimaanishi tupo katika hali nzuri.
Ni kama moja kapata C mwingine F huku passing grade ni B, japo C yupo vizuri kuliko F ila bado hajapass vilevile tu. Watanzania wengi maskini wa kutupa, asilimia kubwa wanaamka hawajui hata kama watafanikisha mlo moja kwa siku, nchi ambazo tunaweza sema ni successful japo wana maskini ndio lakini bado maskini wengi hawasumbuki kwenye swala la msosi.

Tanzania na vyanzo vyote vya fresh water, sehemu ambazo hawana maji salama ya kunywa ni nyingi mno, kuna nchi nyingi tu wanahamu wangekua na vyanzo kama vyetu maana unakuta wana vyanzo kama asilimia 20 ya tulivyonavyo lakini wamefanikiwa ku-supply nchi nzima na maji hayakatiki 24/7. Mwanza tu pamoja na kua na Ziwa Victoria maji yanakatika karibia kila wiki, ni aibu kubwa mno. Bado tunacheza sana

Marais waliopita sisemi wamevuruga sana, wamejitahidi kadri ya uwezo na nawapongeza kwa hilo najua kuongoza nchi sio swala rahisi lakini bado walichokifanya hakitoshi kabisa.
 
Magufuli amezikonga nyoyo zetu lakini atazingonga zaidi kama atatengeneza katiba ambayo kila jambo zuri kwa nchi linazaliwa ndani ya katiba na kila jambo baya kwa nchi linazuiliwa ndani ya katiba. Hatutegemei kwa miaka 5 ya Magufuli ataweza kurekebisha nchi iliyoharibiwa na chama chake kwa miaka 10 ya Mwinyi, 10 ya Mkapa na 10 ya JK, ila anaweza kuchagua vitu vichache tu vya kufanikisha kama vile katiba, ufisadi, afya na elimu tu, na watu watamuelewa tu.

Hata ufisadi itabidi abadilishe baadhi ya sheria. Ufisadi mwingine umehalalishwa kisheria zaidi. Mfano kuwalipa watumishi wa TRA, TPA na BOT mishahara mikubwa kushinda watumishi wengine ni ufisadi uliohalalishwa kisheria. Kwani wao wanatumia mikono minne kutype komputer kwa wakati mmoja?
 
mstari wako wa mwisho umeeleza kila kitu. sio kuponda tu kila kitu. pamoja na kuwa tunailaumu serikali lakini hata sisi wananchi pia sehemu yetu kubwa hatutimizi majukumu yenu. sasa mtu kama wa pwani ambapo maji ni ya uhakika anashindwa hata kujishughulisha kulima mboga mboga na hapo akila mlo mmoja anailaumu serikali. kama sio upuuzi ni nini? mengine tumejitakia wenyewe.

Hehehe mkuu uvivu wa watanzania nalo ni tatizo jingine ambalo kulitatua ni kazi kubwa sana, hilo ndilo jipu la mwisho ambalo kulitumbua litahitaji sindano sijui ya wapi. Watanzania wengi ukweli ni wavivu wanataka wakae waletewe kila kitu kirahisi tu.. Elimu nayo tatizo jingine maana wengi hawana uwezo wa kufikiri wa kukaa wakasema waanzishe biashara na kuplan kila kitu kuhakikisha wanaprogress.
 
Back
Top Bottom