McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 889
- 2,863
Ripoti mpya ya Furaha Duniani (World Happiness Report) ya mwaka 2026 iliyotolewa leo, imeendelea kuipandisha kizimbani Tanzania baada ya kuishikilia nafasi ya chini katika orodha ya mataifa yenye furaha.
Katika utafiti huo uliohusisha nchi 147, Tanzania imeshika nafasi ya 138, ikiingia kwenye kundi la nchi 10 zisizo na furaha zaidi duniani. Licha ya kuwepo kwa ongezeko dogo la alama za tathmini ya maisha (Life Evaluation) kufikia 39.02, hatua hiyo haijatosha kuiondoa nchi hiyo kwenye lindi la majonzi ya kitakwimu.
Source: 2026 World Happiest Countries
Katika utafiti huo uliohusisha nchi 147, Tanzania imeshika nafasi ya 138, ikiingia kwenye kundi la nchi 10 zisizo na furaha zaidi duniani. Licha ya kuwepo kwa ongezeko dogo la alama za tathmini ya maisha (Life Evaluation) kufikia 39.02, hatua hiyo haijatosha kuiondoa nchi hiyo kwenye lindi la majonzi ya kitakwimu.
Yaburuza Mkia Afrika Mashariki
Tanzania imeonekana kusuasua ikilinganishwa na majirani zake wa Ukanda wa Afrika Mashariki. Ripoti hiyo inaonesha kuwa mataifa ya Kenya, Uganda, na Ethiopia yamepiga hatua kubwa zaidi, yakiorodheshwa juu ya Tanzania katika vigezo vya ustawi wa jamii na kuridhika na maisha.Source: 2026 World Happiest Countries