salosalo
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 596
- 278
Kwa muda mrefu watanzania tumekuwa na tabia ya kusifu uovu unapofanyika.... sasa imekwenda hadi makazini. mtu akiajiriwa serikalini kwenye nafasi yoyote yenye mianya ya kuiba au kufisadi bila kufanya hivyo anatukanwa kila aina ya tusi na watz wenzake wanao mzunguka. Zaidi wale waliowahi kushika nafasi za namna hiyo serikalini bila utajiri mpaka kustaafu,wamekuwa wakinyooshewa vidole na kuambiwa Ugoigoi wao ndo uliowaponza.
Lakini kwa wale waliopata kuliibia taifa(kufisadi) kwa namna yoyote wanaitwa wajaja, kwamba huyo sio boya kama maboya wengine. Maneno haya yanazungumzwa mbele ya watoto wanaokua. Wanajegwa kwa kuamini kuwa kuibia serikali ndio ujanja, kinyume na hapo ni uboya. Kumbe naomba jamii tubadilike, tuanye kusifu uchafu huku tukidhani tunajenga kumbe tunabomoa. Tena watu wakiwa kazini ukawazuia kuiba mali ya umma basi watakuundia mikasa ili ufukuzwe kazini kwa madai kuwa unaweka jam. Kwa serikalini kama wanamamlaka kubwa basi maramoja utahamishwa kituo cha kazi.
Nashauri vita dhidi ya ufisadi ianzie nyumbani kwetu. Wazee wa busara semeni kitu hapa....