Tanzania, ufisadi na Mafisadi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania, ufisadi na Mafisadi.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kingu Victor EL, Sep 15, 2011.

 1. K

  Kingu Victor EL Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana Jf nimekuja tena mbele yenu kutaka ufafanuzi kwa Habari kamili inayohusu UKWAPUAJI WA MALI ZA UMA. Ufisadi hapa Bongo land umeanza hivi karibuni ama ulikuwepo hata enzi za Mwalimu. Tujikumbushe kabla ya sherehe za miaka 50 ya --. 1. Ilikuwepo kampuni ya UMA ya usafirishaji mizigo enzi hizo ikiitwa National road haulage. (UMITA) Usafirishaji mizigo Tanzania. Nani anakumbuka kifo cha Kampuni hiyo kilianzia wapi? Kifupi, kifo chake kililetwa na mkataba mbovu kati ya UMITA na kampuni binafsi hewa ya usafirishaji mizigo iliyojiita MWANA KWACHA. 2. Nani anakumbuka kuwa Shirika la ndege la Taifa wakati ule likiitwa AIR TANZANIA CORPORATION. (ATC) lilikodisha ndege mbili mbovu kutoka kwa mfanyabiashara aliyeitwa George Hallack. Ndege hizo hazikufanya kazi kutokana na kukosa hadhi na kutokidhi viwango vya International Air Transport Asossiation. (IATA). Baada ya sakata hilo, serikali kwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana wakati huo mwenyeji wa mkoa wa kati ilikiri na kutamka hadharani kuwa imeshindwa kumpata mmiliki wa ndege hizo hapa duniani kupitia Anwani zake zote. Ndege ziliuzwa kama SCRAPE METAL moja ikiwa KIA na nyingine DIA (uwanja wa Mwl. Nyerere Dar) 3. Tusisahau kivuko cha KIGAMBONI kilichonunuliwa na serikali kwa bei kubwa kama kipya, baadaye kiligundulika kuwa ni KIKUKUU na hakikufanya kazi. Waziri mwenye dhamana alikuwa yuleyule mwenyeji wa mkoa wa mjengoni. Leo tunashangaa Richmond, Dowans na sasa Symbion. UKISHANGAA YA NGELE......... UTAYAONA YA NYAN'GA............. Giza kama kawaaaaaaaaaaa.
   
Loading...