Nimefarijika kusoma reactions za wanaJF kuhusu hili suala linalonikera kila ninaposoma vituko vya kisiasa hapa nchini.
Sina madhumuni ya kushambulia taasisi au viongozi fulani, lakini ili nitoe dukuduku zangu zaidi kufafanua ninavyoona kwamba tunaelekea njia mbaya, niseme tu kwamba hata baadhi ya wale tunaodhani wamejiunga na vyama vya upinzani, wanaonekana wanaanza kusita.
Kwa mfano, kwa nini wakili ambaye najua ni mwanaCDM, asiwe na ujasiri wa kusema kortini kwamba Kova na polisi wanakiuka Katiba yetu ya sasa, kwa kuwatia mbaroni kina Mnyika na Lissu, eti kwa kuhutubia huko Ndago. Ni haki ya chama cha siasa kueneza sera bila bughudha. Saidi Mwema na Kova wapewe hiyo Katiba wasome.
Kitila Mkumbo katiwa mbaroni eti kwa kumkashifu MwanaCCM Mwigulu Nchemba. Mbona hilo ni suala ambalo mwenye kukashifiwa angeenda kortini kudai fidia? Kama kweli Polisi watashirikiana na CCM kugeuza kashfa (slander) kuwa jinai, basi ni lazima tujiulize, tunao uhuru wa mawazo kama Katiba yetu inavyotamka? Tanzania tunadhamiria kukuza demokrasia ya kweli?