Tanzania tunapoteza muda kwenye kujitambua!

Tanzania tunapoteza muda kwenye kujitambua!

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,730
Reaction score
15,387
Watanzania tunapoteza muda mwingi na kuachwa mbali sana kwasababu hatueleweki wala kujitambua tunataka nini kwa nchi yetu.

1. Siasa: Hatujitambui kwamba tunataka mfumo gani. Kuna wanao penda mfumo wa sasa wa vyama vingi ambao hata Nyerere alikuwa ana support. Lakini kumetokea Watanzania ambao hawataki kabisa kuwe na mashindano ya siasa au mfumo wa vyama vingi. Sasa badala ya kupoteza muda, kuongeza uhasama, kufungana bila sababu, kuaibisha vyombo vya usalama na hata mahakama. Ni bora kama nchi tuamue tunataka nchi ya namna gani. Kusingiziana singiziana makosa haitasaidia nchio yetu kuwa na maendeleo. Kibaya zaidi kumeanza kuwa na matabaka ya maoni kwa sehemu na hii itarudisha nyuma nchi yetu maana hakuna umoja kwenye maendeleo bila kukubaliana mfumo. Mfano mzuri ni Arusha serikali na wananchi wako tofauti kwasababu ya vyama. Wanaosema maendeleo hayajali siasa wako kweli lakini maendeleo yanajali mfumo na sasa tuna mfumo mmoja lakini wasioupenda wanatumia sheria ambazo si za kikatiba kuupinga na hii ni kwa kubambika kesi na kuzuia uhuru wa habari pale unapo tofautiana nao.

2. Elimu: Sio siri elimu yatu inashuka sana na tukitoa siasa angalia certifications watoto wetu ukilinganisha na zamani international certification watoto hata wana vyuo wana fail zaidi kuliko wanafunzi wa miaka 1990's ukilinganisha Form 6 ya mwaka 1996,95,94 kwenye shule yeyeote hata kama Ilboru halafu uangalie hata waliopata div 1 uwape test hawataweze kuwa na score kama wenzao wa sasa. Tatizo kubwa ni kwamba hatujui tufuate mfumo gani kila uongozi ukija unabadilisha mfumo wa shule. Kwasababu ya technologia tunazidi kuachwa mbali na wenzetu na tuna mfumo wa elimu ambao hauendani na kazi za siku hizi. Elimu ni zaidi ya madawati na majengo. Wenzetu elimu inazidi kuwa rahisi maana sasa hata vitabu unaweza kupata kirahisi. lakini bado hatujawa wabunifu . Hivyo kama nchi tuweke mfumo wa elimu wenye ushindani , utakao endana na kazi za siku hizi na mfumo utakao leta maendeleo na tuweke siasa pembeni. Hatuwezi kuwa na mfumo ambao unabadilika kila waziri mwingine akichaguliwa


Kuna mengi lakini Watanzania inaelekea hatujui tunataka nini na tunatakiwa kujitambua mapema kama nchi ili twende pamoja. Hatuna mfumo hata kwenye sehemu moja ambao unaeleweka hata kwenye viwanja, afya, bank, ....... na hii inaturudisha nyuma sana
 
Back
Top Bottom